SIFA ZA MABANDA YA KUFUGIA KUKU
Banda la kuku |
Katika ufugaji wa kuku itakiwa kuwa na ubunifu wa banda la ufugiaji kuku ili kuboresha uzalishaji wa kuku bora wenye afya nzuri na wasiweze kushambuliwa na magonjwa mbalimbali kwa mazingira ya mabanda yakiwa ayana ubora ni tatizo.
Kuna watu wameweka fikra za ufugaji lakini awazii banda la kuwaweka kuku linatakiwa likizi vitu gan ili aweze kufuga.
SIFA ZA BANDA ZURI LA KUKU:
- kuwe na hewa yakutosha kwenye ilo banda.
- kuwe na mwanga wakutosha
- liwe na uwezo wakupitisha mionzi ya jua(miyale ya jua)inayo chomoza maghalibi ya banda lako na mashariki ya banda
- lenye ukubwa mzuri ambao inategemea na kuku unaotaka kufuga
- n.k
Hewa ni muhimu kwa kila
kiumbe, hivyo banda la kuku ni lazima liingize hewa safi na kutoa ile chafu na
liweze kuingiza mwanga wa kutosha.
1. Kwa kifupi ni kwamba
madirisha ya banda ni lazima yawe makubwa na ya kutosha ili yaingize hewa safi
na kutoa ile chafu.
2. Ni vema madirisha haya
yawe juu kiasi cha meta moja (1) kutoka chini ili hewa ipite juu ya vichwa vya
kuku.
3. Hewa safi siyo upepo,
hivyo jaribu kuzuia upepo mkali kuingia ndani ya banda la kuku ama sivyo kuku
wataugua ugonjwa wa mafua na niumonia na vifaranga vinaweza kufa kwa ugonjwa wa
baridi.
4. Jenga Banda lako kwa
kukinga upepo unakotokea na kupanda miti kuzunguka banda hilo la kuku ili
kupunguza kasi ya upepo na kuweka kivuli dhidi ya jua kali na joto.
UKAVU
NA USAFI WA NDANI:
Kwa vile kuku si ndege wa
majini kama bata , ni jambo la busara kuhakikisha kuwa mahali anapoishi hapana
unyevunyevu.
1. Banda la kuku lijengwe mahali palipoinuka ili kuzuia maji ya
mvua yasiingie.
2. Wajengee kuku uchaga wa
kulalia kwa kuweka viguzo vyenye urefu wa meta moja na kutandika miti juu yake
ili usiku walale hapo, kuliko kuwalaza ardhini au sakafuni.
3. Ukavu wa banda ni muhimu
sana hasa kwa vifaranga na kuku wanaotaga. Ndani ya banda lenye unyevu mayai
kuchafuka sana hata wakati mwingine huoza kwa urahisi na jitihada zako zitakuwa
ni bure.
4. Sakafu ya banda ni vizuri
ikawa ya zege lakini kutokana na uhaba wa fedha sakafu inaweza kutengenezwa kwa
mabanzi (mabanda yaliyoinuliwa) au udongo mgumu na au mchanga ambao utafunikwa
kwa mabaki ya taka za mpunga na yale ya mbao.
5. Ili kuepuka unyevunyevu
ni vyema eneo/mahali pla kujenga banda pawe pameinuka na penye kupitisha hewa
ya kutosha.
PAA
LA BANDA:
Paa la banda liwe madhubuti
ili kuzuia maji ya mvua kuingia hasa wakati wa masika. Sakafu ya banda iwe juu
zaidi ya usawa wa nje. Paa linaweza kuezekwa kwa mabaki ya vipande vya bati ,
madebe na kama ikishindikana tumia nyasi zinazofaa kwa ajili ya kuezeka nyumba
katika eneo hilo.
MATANDIKO
Nilazima kuweka matandio
katika sakafu ya banda la kuku. Sehemu ambayo kukuwakubwa wanaweza kutagia. Ni
vizuri kutumia maranda, na si Pumba zinazo tokana na mbao
Kuku wanaweza kula pumba za
mbao. Kwa kuku wanaohatamia, vipande vidogo na vilaini vya miti na makapi kama
vile pumba za mpunga zinaweza kutumika
NAFASI
YA KUFANYA KAZI:
Banda la kuku lisiwe na
nguzo au mbao nyingi sana ndani kiasi cha kumfanya mhudumiaji wa kuku ashindwe
kufanya kazi zake. Hali hiyo itamfanya apoteze muda mwingi katika kuzizunguka
nguzo hizo, hasa wakati wa kuokota mayai au kufanya usafi.
VIFAA:
Unapotaka kujenga banda la
kuku kwanza kabisa tayarisha vifaa vinavyotakiwa. Vitu kama miti au nyasi,
nyavu au fito, misumari au kamba ni muhimu kuviandaa mapema.
Pili ni lazima uwe na
plani/ramani kamili ya banda hilo. Kwa wastani kila kuku anahitaji nafasi ya
Meta za eneo la 0.11 hadi 0.22 (futi 1 hadi 2 za eneo.) kutegemeana na umri wa
kuku.
UJENZI
RAHISI:
Kuku wafugwao hatimaye ni
lazima wafidie gharama za Ujenzi wa mabanda na chakula. Gharama zikiwa kubwa
sana huenda ukaifanya shughuli ya ufugaji isiwe na faida hata kidogo hali hiyo
itamfanya mfugaji aone ufugaji hauna maana yoyote kwake. Lakini ukijenga banda
lako kwa kutumia vifaa vinavyopatikana kwa urahisi utaongeza faida zaidi
kwakuwa umepunguza gharama za uendeshaji wa mradi.
VIPIMO:
Banda la kuku linatakiwa
liwe na Meta 15 hadi meta 22 za eneo yaani Meta 3 hadi 4.5 za upana kwa meta 5
za urefu. Banda hili linaweza kutunza kuku 100 wakubwa kwa wakati mmoja.
HITIMISHO:
• Ujenzi wa mabanda
unasisitizwa katika kuboresha ufugaji wa kuku wa asili ili;
• Kuongeza uzalishaji na
kupunguza vifo vya vifaranga kwa majanga mbalimbali kama vicheche, mwewe, mapaka,
mbwa na wizi wa kuku wanaozurura holela.
• Vile vile inatarajiwa
kwamba kuku wanaozuiliwa kwenye banda na kuwekewa chakula mchanganyiko
wataongeza uzalishaji kwa kiasi kikubwa.
MIFANO YA MABANDA BORA
Hii ni mifano ya mabanda
bora ya kuku yanayotengenezwa Tanzania na yanafaa zaidi kwa wafugaji
wenye maeneo ya mijini ambako maeneo ya ufugaji ni shida zaidi.
safi, na nimevutiwa na Maelezo mazuri kabisa... je naweza kumpata fundi mzuri atakaye weza kunijengea banda zuri na la kisasa? namba zangu ni 0713-453532
ReplyDelete