FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU


Unaweza kuzidharau mbegu za maboga, lakini ni miongoni mwa mbegu zenye faida kubwa mwilini, zinazoweza kuzuia na kutibu hata magonjwa hatari yaliyoshindikana hospitalini.
Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi uliokwishafanyika, zifuatazo ni faida za kifya mtu anazoweza kuzipata kwa kula mbegu za maboga, zikiwa mbichi ama zilizokaangwa:
HUIMARISHA MOYO, MIFUPA
Mbegu za Maboga (Pumkin Seeds), zina kiwango kingi cha madini aina ya Magnesium ambayo ni muhimu kwa afya ya moyo, uimarishaji mifupa, mishipa ya damu na ufanisi wa utumbo mpana. Magnesium imeonesha uwezo mkubwa wa kuzuia mshituko wa moyo na kiharusi
.
KINGA YA MWILI
Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini aina ya Zinc, ambayo yana faida nyingi mwilini, zikiwemo uimarishaji wa kinga mwilini, ukuaji wa seli, macho na ngozi ya mwili. Vile vile Zinc huimarisha nguvu za kiume.
SARATANI YA KIBOFU
Kutokana na kuwa na kiwango kingi cha Zinc, utafiti umeonesha kuwa mafuta na mbegu zenyewe za mabogo huweza kutumika kama dawa ya kutibu saratani ya kibofu.
KINGA YA KISUKARI
Utafiti umeonesha pia kuwa mbegu za maboga huweza kuimarisha utokaji wa ‘insulin’ mwilini, hivyo kuwa kinga au kuleta ahueni kubwa kwa wagonjwa wa kisukari.
TIBA KWA WALIOFIKIA UKOMO
Mafuta ya mbegu za maboga hayana madhara, zaidi yana kirutubisho muhimu cha kurekebisha Cholesterol mwilini, kushusha shinikizo la damu, kuzuia uvimbe, maumivu ya kichwa, maumivu ya viungo vya mwili na vile vile huondoa maumivu mbalimbali yanayowapata wanawake wenye umri mkubwa waliofikia ukomo wa hedhi (Menopause).
UGONJWA WA INI
Mbegu za maboga pia zina kamba lishe na kinga kubwa ya kupambana na magonjwa nyemelezi. Mbali na hayo, mbegu zina virutubisho vinavyotoa kinga dhidi ya magonjwa ya ini na moyo.
USINGIZI
Kwa watu wenye matatizo ya usingizi, wanashauriwa kula punje kadhaa pamoja na tunda lolote muda mfupi kabla ya kupanda kitandani, utafiti umeonesha kuwa mbegu za maboga zina kirutubisho kinachochea uzalishaji wa homoni za usingizi kwa wingi.
UVIMBE
Mbegu za maboga zimeonesha kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuzuia magonjwa yote ya uvimbe mwilini, yakiwemo ya kuvimba miguu, vidole na hata majipu.
JINSI YA KULA MBEGU
Hakikisha unakula mbegu ambazo hazijaoza na zilizosafi ambazo hazijakaa muda mrefu. Kwa usalama zaidi, zioshe kwa maji safi kisha zianike, inapendeza zaidi ukila bila kukaanga, lakini pia ukiamua kula za kukaanga bado utapata faida zake, muhimu usiziunguze wakati wa kukaanga. Kwa kawaida hukaangwa kwa muda usiozidi dakika 10 tu.

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

UMUHIMU WA KUJIFUNZA SAIKOLOJIA