Posts

MADAM RITA AFUNGUKA KWA SABABU ZILIZOMFANYA AIHAMISHIE BONGO STAR SEARCH TBC 1

Image
  Epiq Bongo Star Search ya mwaka 2013 haitaoneshwa tena kupitia ITV. Mwaka huu shindano hilo la kusaka vipaji vya kuimba litakuwa likioneshwa kupitia TBC1.  Kupitia Facebook, Rita Paulsen aka Madam Rita ambaye ni mwanzilishi na jaji mkuu wa shindano hilo ametoa sababu mbili za kuhamisha matangazo hayo kutoka ITV hadi TBC1. “Baada ya kusoma maoni yenu, ningependa kufafanua sababu mbili za kurusha Epiq Bongo Star Search 2013 kupitia kituo cha Televisheni cha TBC1.  Kwanza kabisa ni sababu za kibiashara ndio zimepelekea kipindi cha EBSS kurushwa kupitia TBC1 na sababu ya pili ni kwamba baada ya kwenda kidigitali, TBC1 sasa inapatikana kwenye ving’amuzi karibia vyote vikiwemo Star Times, DSTV na Zuku.”Ila kwa wawle wanao tumia madishi au mfumo wa analogia watashindwa kuona mzshindano aya mwaka kupitia kubadilisha utalatibu wa kurusha kipindi cha Epiq Bongo star search

UJIO WA TOFAUTI WA MWANAMUZIKI NAY WA MITEGO KUTOA MAKAVU KWA ZITO KABWE

Image
Mfalme wa kudiss Tanzania, Nay wa Mitego amerejea tena kuchafua hali ya hewa kwa kutengeneza mijadala kwenye radio na kwenye mtandao kwa ngoma yake mpya, Salam Zao. Kwenye Salam Zao, Nay ameendeela kufanya kile akifanyacho kwa uzuri (do what he does best) kuponda.   Awamu hii list ya aliowadiss imeongezeka zaidi na kuingia pia kwenye siasa huku akiendelea kuwapa madongo wana hip hop wenzie. Ameanza kwa kumdiss Madee kwa kusema kuwa yeye ndio rais wa Manzese na kwamba Madee amesanda. “Mi ndo rais wa Manzese yule tozi kasanda, Manzese mikono juu naiongoza kamanda,” anachana Nay. Nay wa Mitego ameendelea kuwadiss wana hip hip huku akiijita kuwa yeye ndio gangster rapper na anatengeneza hela huku wengine wakinuka vikwapa. Hakusita pia kuwarushia bombshell Weusi. “Yo Mchomvu wape salam ‘Kubumkubum’ waimbie watakufa njaa muziki umebadilika,” anarap Nay. Nay pia amemdiss Zitto Kabwe kwa kurap:    “Word up Diamond, mwanangu wewe si mtoto ...

BARNABA SABABU ZILIZOMFANYA KUTEMANA NA SHILOLE

Image
Baada  ya   siku  nyingi  kupita  tangu  Shilole  na  Barnaba  watemane,imebainika  kuwepo  kwa  siri  kubwa   zilisababisha  wawili  hao  watemane .... Chanzo  cha  karibu  na  Barnaba  kimedai  kuwa  sababu  zilizosababisha  wawili  hao  kutemana   ni  pale  shilole  alipodanganya  umri  wake  na  kumwachia  Barnaba  jukumu  la  kumlelea  watoto  wake... "Suala  la  kulea  watoto  wasio  wa  kwake  lilikuwa  ni  gumu  sana   kwa  Barnaba  kwani  wakati  huo  ndo  kwanza  alikuwa anaanza  maisha na  hakuwa  na uwezo  wa  kumhudumia  mtu  na  wanae" ..Kilisema  chanzo  hicho. Chanzo  hicho  kiliendel...

Fahamu mambo mengi kuhusiana na Ndizi kuwa sehemu ya maisha yako.

Image
Ndizi ni tunda ambalo limezoeleka kwa watu wengi , linapatikana karibu kila mahali . Hata hivyo inawezekana ukawa hujafahamu umuhimu wa tunda hili mwilini mwako . Taarif aifuatayo itabadilisha mtazamo wako kwa tunda hili na utafahamu kwanini hupaswi kulichukulia poa hata siku moja . Ndizi mbivu zina sukari zinazohitajika kwenye mwili wako , sukari hizi ni zile ambazo zinafahamika kwa majina ya kitaalamu ya Sucrose , Fructose na Glucose ambazo kwa pamoja zimechanganyikana na Fibre muhimu ambazo zinalifanya tunda hili kuwa chanzo muhimu cha nishati au nguvu inayohitajika mwilini mwako . Utafiti umeonyesha kuwa ndizi mbivu mbili zinatosha kukupa nishati ambayo utaitumia kwa mazoezi ya nguvu ya dakika 90 ambazo ni sawa na saa moja na nusu . Hii ndio sababu wanamichezo wengi hutumia ndizi mbivu kabla na baada ya mazoezi mazito na wakati mwingine kabla na baada ya mashindano katika mchezo husika . Nishati si faida pekee inayokuja kwenye tunda la ndizi , tunda hili lin...

Jipya lililosemwa na Serikali kuhusu kodi ya simcard Tanzania

Image
Ni kuhusu kauli ya serikali kuhusu ile ishu iliyochukua sana headlines ya kodi ya simcard Tanzania ambapo kwenye Exclusive na Gazeti la Nipashe, Waziri wa fedha katoa ya moyoni. Anakwambia Serikali imekubali kwamba kodi mpya ya laini ya simu ni mgogoro na inakusudia kurejesha muswada wa sheria ulioanzisha kodi hiyo bungeni kwa mjadala zaidi kuanzia mwishoni mwa mwezi ujao. Kingine alichosema ni hiki… ‘hili swala kwa sasa linashughulikiwa kwa mapana zaidi na Serikali na linatarajiwa kupelekwa bungeni kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi, Wabunge watapata nafasi ya kulijadili na muafaka utapatikana’  wakati hiyo kauli ikitoka kwa Waziri wa fedha, leo utaratibu wa makato ya laini ya simu kwa shilingi elfu moja unatarajiwa kuanza kwa kampuni zote za simu Tanzania

KAULI YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ITAMFIKISHA KORTINI"WAPIGWE TU"

Image
KAULI ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ya kubariki vyombo vya dola kuendeleza kipigo kwa raia wanaokaidi amri imechukua sura mpya baada ya Kituo cha Sheria na Haki za Bindamu (LHRC) kutangaza kumburuza mahakamani wiki hii kutokana na kushindwa kufuta kauli yake. Juni 20, mwaka huu, wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo bungeni, Waziri Mkuu, Pinda, alivitaka vyombo vya dola kuendelea kuwapiga raia, akisema kuwa hakuna namna nyingine kwani serikali imechoka. Kauli hiyo imekuwa ikipingwa na wananchi, mashirika ya kutetea haki za binadamu na wanasiasa wakimtaka Waziri Mkuu, Pinda, kuifuta kwa kuomba radhi, wakidai kuwa inachochea uvunjifu wa sheria. Akitangaza kusudio la kituo hicho kufungua kesi dhidi ya Pinda, Mkurugenzi wa maboresho na utetezi, Harold Sungusia, alisema hadi jana walikuwa tayari wameandaa kusudio la shtaka lao. Alisema kuwa kisheria kilichowafanya kufikia uamuzi huo ni kutokana na waziri mkuu huyo kukiuka Katiba ya nchi inayozungumzia u...

MWANAMUZIKI KALA JEREMIAH NAYE KAFUNGUKA KUMPIGIA KAMPENI LOWASSA....ANADAI KUWA LOWASSA NI JEMBE

Image
Msanii wa Hip Hop na mshindi wa tuzo 3 za KTMA 2013, Kala Jeremiah amefunguka kwa kuandika waraka mrefu kuelezea jinsi anavyomkubali waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kwamba anafaa kuiongoza nchini. Usome waraka wake huo wote; Mimi Kala Jeremiah nilikuwa msanii wa kwanza Tanzania kumsema mheshimiwa Edward Lowassa kupitia wimbo wangu uitwao wimbo wa taifa baada ya mheshimiwa kukumbwa na kashfa ya ufisadi wa Richmond. Kwa kipindi kile kila mmoja wetu alihamaki sana na kuona kweli mzee wa watu ni fisadi.Kwenye wimbo huo kuna mistari nilisema, ‘mi siyo mwana siasa sisubiri tume ichunguze nistaafu ka Lowassa. Kwa kuwa mimi ni mzuri sana kwenye kufanya uchunguzi binafsi nilitumia muda mwingi sana kulichunguza swala hili la kashfa hii na baadae niligundua kuwa ni swala la kisiasa, na yalikuwa ni mapito ambayo mwanadamu yoyote hupewa muda wa kupitia magumu ili kupimwa imani yake kwa Mungu. Baada ya kugundua hayo mwaka jana nilitengeneza wimbo unaoitwa ...