Fahamu mambo mengi kuhusiana na Ndizi kuwa sehemu ya maisha yako.


Ndizi ni tunda ambalo limezoeleka kwa watu wengi , linapatikana karibu kila mahali . Hata hivyo inawezekana ukawa hujafahamu umuhimu wa tunda hili mwilini mwako . Taarif aifuatayo itabadilisha mtazamo wako kwa tunda hili na utafahamu kwanini hupaswi kulichukulia poa hata siku moja .
bananas-3banana-amazing-fruit-and-cure
Ndizi mbivu zina sukari zinazohitajika kwenye mwili wako , sukari hizi ni zile ambazo zinafahamika kwa majina ya kitaalamu ya Sucrose , Fructose na Glucose ambazo kwa pamoja zimechanganyikana na Fibre muhimu ambazo zinalifanya tunda hili kuwa chanzo muhimu cha nishati au nguvu inayohitajika mwilini mwako .

Utafiti umeonyesha kuwa ndizi mbivu mbili zinatosha kukupa nishati ambayo utaitumia kwa mazoezi ya nguvu ya dakika 90 ambazo ni sawa na saa moja na nusu . Hii ndio sababu wanamichezo wengi hutumia ndizi mbivu kabla na baada ya mazoezi mazito na wakati mwingine kabla na baada ya mashindano katika mchezo husika .
Nishati si faida pekee inayokuja kwenye tunda la ndizi , tunda hili lina faida nyingine ambayo ni kuusaidia mwili wako kupambana na kujikinga na maradhi  kadhaa.
Msongo wa Mawazo/Mfadhaiko wa akili(stress & Depression)
Kwa mujibu wa tafiti kadhaa , watu wengi wanaopata mafadhaiko au msongo wa mawazo hujisikia nafuu pale wanapokula ndizi mbivu . Hii ni kwa sababu ndizi mbivu  zina virutubisho aina ya TRYPTOPHAN ambayo ni aina ya protini ambayo mwili huigeuza na kuwa SEROTONIN ambayo kazi yake ni kukufanya upate utulivu na kukurejesha katika hali ya kawaida mpaka utakapota furaha na kuondokana na msongo wa mawazo . Zaidi ya hapo ndizi huongeza Vitamini B6 mwilini  ambayo inasimamia usambazaji wa glucose au sukari mwilini na hivyo kusaidia kutuliza msongo wa mawazo .

 Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
Ndizi zina madini ya chuma  na zinasaidia uzalishaji wa haemoglobin ambayo ni mzalishaji mkuu wa damu mwilini  hivyo inawasaidia wale wenye matatizo ya upungufu wa damu mwilini.

Presha ya Damu.
Ndizi mbivu zina madini ya Potasium na ina madini ya chumvi kwa kiwango cha chini  jambo ambalo linafanya tunda hili kuwa dawa ya kupambana na matatizo ya presha . Mamlaka ya chakula na dawa nchini marekani imetambua uwezo wa ndizi katika hili kiasi cha kuagiza wazalishaji na viwanda vya ndizi kufanya tunda hili kuwa rasmi katika mapambano ya kupunguza vifo vitokanavyo na presha na kiharusi(stroke)

Nguvu ya Ubongo/Akili(Brain Power)
Katika utafiti uliofanywa huko Twickenham (Middlesex) nchini Uingereza wanafunzi 200 walifaidika kwa kufaulu mitihani yao mwaka huu kwa kula ndizi mbivu katika milo ya asubuhi  na mchana . Ndizi imebainika kuwa na uwezo wa kuusaidia ubongo kuongeza nguvu yake . Utafiti umeonyesha kuwa madini ya Potassium yanaweza kusaidia ubongo kuwa na kasi na uwezo zaidi ya hali ya kawaida .

Kufunga Choo(Constipation)
Fiber inayopatikana kwenye ndizi mbivu inaweza kuurejesha utumbo ambao umesababisha kufunga choo kufanya kazi kama kawaida .

 Madhara ya matumizi ya kilevi(Hangover)
Moja ya njia za haraka za kurudi kwenye hali ya kawaida baada ya kupata madhara ya matumizi ya kilevi hasa asubuhi unapoamka ni kutumia ndizi au bidhaa zitokanazo na ndizi kama vile Banana Milkshake . Ndizi hutuliza tumbo na inajenga au kurejesha kiwango cha kawaida cha sukari mwilini huku ikirutubisha mfumo wa maji mwilini .

Kiungulia (Heartburn)
Ndizi zina uwezo wa kupambano na kemikali au acid zinazosababisha kiungulia , jaribu kula ndizi na utakuwa shahidi katika hili.

 Kuumwa asubuhi kwa kina mama wajawazito(Morning Sickness)
Matumizi ya ndizi yamegundulika kusaidia kuepusha kuugua asubuhi ambako kunawapata kinamama wajawazito , hii ni kutokana na uwezo wa tunda hili wa kucontrol kiwango cha sukari mwilini.

Alama za Kung’atwa na Mbu.
Kwa wale wanaotokwa na vile vipele vidogo vyekundu baada ya kung’twa na mbu , jaribu kufuta eneo lenye kipele kama hicho kwa upande wa ndani ya ganda la ndizi , ni ajabu lakini hufanya kazi kwa kuwa hii hupunguza uvimbe na muwasho.

Neva (Verves)
Ndizi zinasaidia sana kutibu mfumo wa neva (nervous system).
Hata kwa wale watu wenye matatizo ya uzito ambao unatokana na tabia zisizo za salama za ulaji hasa kutokana na kukosa muda wa kula na kulazimika kula vyakula vyenye mafuta  mengi vinavyopikwa haraka ndizi inaweza kuwa msaada mkubwa . Utafiti uliofanywa kwa watu 5000 ambao walikuwa wagonjwa wa hospitalini walipata nafuu ya matatizo yao kwa kutumia ndizi kila baada ya saa mbili .

 Vidonda vya tumbo .(Ulcers)
Ndizi zinatumika kama chakula ambacho kinaweza kuwa na msaada kwa watu wenye matatizo kwenye utumbo, hii ni kutokana na ulaini wake na hupunguza acid ambayo inasababisha vidonda tumboni  na pia hupunguza maumivu kutokana na kuziba baadhi ya vidonda hivyo .

 Kupunguza hali ya joto mwilini.
Ndizi ni tunda ambalo huweza kusaidia kupunguza joto . Nchini Thailand kina mama waja wazito hula ndizi ili kuhakikisha wanawazaa watoto wao katika hali ya joto pungufu .
Banana_stand_near_Lake_Manyara_Tanzania_DP392
Hivyo basi ndizi ni tunda ambalo lina uwezo wa kusaidia matatizo mengi ya afya ya mwanadamu . Unapolifananisha na Apple ndizi inazidi tunda hili kwa protini kwa angalau mara nne , madini ya wanga au carbohydrates mara mbili , madini ya fosforasi mara tatu ,Vitamini A na madini ya chuma mara tano , na mara mbili kwenye vitamin nyingine na madini . Ni muda wa kubadili ule msemo usemao Apple moja kwa siku hukuweka mbali na daktari na kuufanya kuwa Ndizi moja kwa siku hukuweka mbali na daktari au hospitali.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

NINI MAANA YA MAPENZI

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU