Jipya lililosemwa na Serikali kuhusu kodi ya simcard Tanzania
Ni kuhusu kauli ya serikali kuhusu ile ishu iliyochukua sana headlines ya kodi ya simcard Tanzania ambapo kwenye Exclusive na Gazeti la Nipashe, Waziri wa fedha katoa ya moyoni.
Anakwambia Serikali imekubali kwamba kodi mpya ya laini ya simu ni mgogoro na inakusudia kurejesha muswada wa sheria ulioanzisha kodi hiyo bungeni kwa mjadala zaidi kuanzia mwishoni mwa mwezi ujao.
Kingine alichosema ni hiki… ‘hili swala kwa sasa linashughulikiwa kwa mapana zaidi na Serikali na linatarajiwa kupelekwa bungeni kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi, Wabunge watapata nafasi ya kulijadili na muafaka utapatikana’
wakati hiyo kauli ikitoka kwa Waziri wa fedha, leo utaratibu wa makato ya laini ya simu kwa shilingi elfu moja unatarajiwa kuanza kwa kampuni zote za simu Tanzania
Comments
Post a Comment