BARNABA SABABU ZILIZOMFANYA KUTEMANA NA SHILOLE



Baada  ya   siku  nyingi  kupita  tangu  Shilole  na  Barnaba  watemane,imebainika  kuwepo  kwa  siri  kubwa   zilisababisha  wawili  hao  watemane ....

Chanzo  cha  karibu  na  Barnaba  kimedai  kuwa  sababu  zilizosababisha  wawili  hao  kutemana   ni  pale  shilole  alipodanganya  umri  wake  na  kumwachia  Barnaba  jukumu  la  kumlelea  watoto  wake...

"Suala  la  kulea  watoto  wasio  wa  kwake  lilikuwa  ni  gumu  sana  kwa  Barnaba  kwani  wakati  huo  ndo  kwanza  alikuwa anaanza  maisha na  hakuwa  na uwezo  wa  kumhudumia  mtu  na  wanae"..Kilisema  chanzo  hicho.

Chanzo  hicho  kiliendelea  kufunguka  kuwa  Shilole  ndiye  aliye  mtongoza  Barnaba  kwa  staili  ya  kumdanganya  umri  huku  akimweleza  kuwa  swala  la  watoto  wake  lilikuwa  linasimamiwa  na  baba  yao.

Habari  zinadai  kwamba, baada  ya  Barnaba  kuingizwa  mkenge, penzi  lao  lilikuwa  kwa  kasi  sana  huku  Shilole  akijitahidi  kuuficha  ukweli  kwa  muda  mrefu.


"Cha  ajabu  ni  kwamba, kadri  siku  zilivyozidi  kusonga  mbele, Shilole  alijisahau  na  kuanza  kumwachia  mzigo wa  kuilea  familia  yote..

"Aidha, Shilole  aliusahau  uongo  wake  na  akajichanganya  kutoa  historia  ya  maisha  yake  katika  gazeti  moja  la  udaku ambako  alitaja  umri  wake  halisi  huku  akisimulia  jinsi  alivyobakwa  hadi  kupata  mimba .Jambo  hilo  lilimstua  sana  Barnaba"..Kilisema  chanzo  hicho  na  kuongeza:

"Kipengele  cha  kubakwa  kilimchanganya sana  Barnaba  akawa  anajiuliza, kama  alibakwa  na  kupata  mtoto,matunzo  ya  mtoto  anayapataje  kwa  mtu  aliyembaka

"Tukio  hilo  lilo  lilimfanya  Barnaba  apoteze  imani  na  ndipo  alipoanza  alipoanza  kutafuta  visa  vya  kumtema  Shilole"

Shilole  alipotafutwa  kuzungumzia  suala  hilo  hakuweza  kutoa  ushirikiano  wa  kutosha.


Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

NINI MAANA YA MAPENZI

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU