Ombi Hili la Wema Sepetu, Likufikiae na Wewe….Tubadilike

“Watanzania wenzangu, naombeni leo tujiulize: mitandao ya kijamii ina kazi gani kama sio kuelimisha, kuendeleza na kunufaisha jamii?

Huu ni mwaka 2015. Kama kupendana bure, tushapendana vya kutosha. Kama kutukanana bila sababu, tushatukanana vya kutosha. Kama kushabikia vitu ambavyo havina msaada wowote kwa sisi na familia zetu, tushashabikia vya
kutosha.

Imefika hatua ya kunyanyuana, sio kushushana. Kuelimishana, sio kusemana. Kupeana moyo, sio kukatishana tamaa.

Imefika hatua ya kutegemea mabadiliko, na kupigania mabadiliko.

Nakuomba wewe kaka angu, dada angu, mama angu, baba angu...nakuomba ufanye maamuzi leo, kwamba kesho yako haitakua kama jana yako.

Kwa jina naitwa Wema Sepetu. Na leo hii nimeamua kwamba kesho yangu, haitakua kama jana yangu!

Wewe je? “.-Wema  mwenye followers zaidi ya laki nne mtandaoni ameandika haya na kuungwa mkono na mashabiki wengi na hata wale wanomdisi.

Asante sana Wema, ujumbe umefika.

Kwa jina naitwa Mzee wa Ubuyu  na leo hii nimeamua kesho yangu haitakauwa kama jana yangu.

11.03.2015 -  Tags:  WEMA

No comments:

Post a Comment

Search This Blog

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

NINI MAANA YA MAPENZI

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU