MPENZI WAKO NDIYE ADUI WAKO...
MPENZI WAKO NDIYE ADUI YAKO
IMEANDIKWA NA
MLAWA,S.S
MAPENZI
Kila binadamu
hupenda jambo fulani. Mapenzi ya mtu juu ya jambo yaweza kumvutia kiasi kwamba
anaweza kupoteza welekeo wa maisha yake. Watu hupenda hadi kileleni. Hapa ndipo
mtu aelewi hili wala lile. Hali hii si tu kwa vijana wanaoingia katika umri wa
balehe bali hata kwa wale waliovuka umri huu. Kweli kila mtu anahaki ya
kupenda. Na mapenzi haya yalianza pale binadamu walipoanza kuishi pamoja kama
mke na mume kama vitabu vyetu vya dini
vinavyoelekeza, ambavyo ni Biblia na Kuruhani.
Napenda kuwa
muwazi sana juu
ya aina ya penzi ninalozungumzia. Ni yale mahusiano ya kimwili yaliyopo kati
mwanamke na mwanaume. Haya ndiyo mahusiano ninayozungumzia na sizungumzii yale
ya watu wa jinsia moja. Mapenzi hayauzwi na ayachagui rangi wala kabila.Mapenzi
ni kitu asilia ambacho humkuta mtu juu
ya mtu mwingine ambaye anaweza kuwa mwanamke kwa mwanaume au kinyume chake. Na
hawa kila mmoja hutokea kumpenda mwenzake mpaka kufikia kilele cha penzi.
Angalia mfano
huu; umepita wapi na kutembea mikoa mbalimbali au wilaya, tarafa, kata, vijiji
na mitaa mingapi? Umekutana na wangapi wazuri (wanawake au wanaume), na
ulimpenda yupi. Inawezekana kati ya uliowachagua hakuna hata mmoja kati ya wale
uliokutana nao ukaridhia kuwa naye. Lakini ulikutana na kijana mmoja ambaye
amekuvutia sana
zaidi ya asana na mahusiano ukaanza kuanzisha mpaka leo ni mke wako au mchumba
wako. Hapo ndipo ninaposema “love is something natural” na si
kitu cha kubahatisha tu.
Na ieleweke kwamba mke mzuri ni wako tu, na
mme mzuri ni wako tu. Hakuna ubishi kwa hili. Na pale unapoona kuwa mke au
mme wako si mzuri basi ulikosea wakati wa uchaguzi wako. Hapo huna budi kuonyesha unampenda kama kitabu hiki kinavyoeleza uk.6 & 7. Na ujue
kwamba kila mtu ana haki ya kupendwa na mme, mke au mchumba wake. Penye upendo pana mapenzi ya kweli.
NINI MAANA YA MAPENZI?
Neno mapenzi ni pana sana. Na kila mtu huweza kufikiri kulingana
na uelewa wake juu ya mapenzi kati ya mtu na mtu. Mapenzi ni ile hali asilia
ambayo mtu anakuwanayo kwa mtu mwingine na inapaswa kuwa na makubaliano baina
ya wahusika ambayo yaweza kuwa ya muda mfupi au muda mrefu. Wengine husema
mapenzi ni ile hali ya mtu kuwa na mahusiano ya kimwili na mwingine.
Kipindi
tulichopo sasa ni kipindi cha utandawazi.
Si mtoto mdogo si wakubwa wote wanayafahamu mapenzi yalivyo. Kwa sasa imekuwa
kawaida kwa kila mtu kuanza uhusiano hata kabla ya kufunga ndoa. Hii ndiyo
ninayoita utandawazi. Watoto wadogo hupata habari hizi kupitia masimulizi
kutoka kwa kaka na dada zao nyumbani au nje. Hii haikuwa tamaduni yetu, lakini
sasa ni jambo la kawaida kwa mwanafunzi wa darasa la tano kukutwa na ujauzito.
Lakini ni kwa mazingira hayahaya.
Kipindi hiki
ndicho kipindi kigumu kwa vijana kujua yupi ni mke/mme mwema na yupi si mke/mme
mwema. Athari hizi huwakuta sana
akina dada ambao wakizidisha miaka ishirini na saba, yule ambaye alikuwa mme
mzuri anampoteza ndani ya miaka 18 hadi miaka ishirini. Ndani ya miaka hii
mwanamke huvutia na anaonekana kama ua
linalovutia wadudu (Dr Isack Ndodi, 2011). Nakubaliana sana na maneno ya Dr. Ndodi akizunguma Channel 5 kati ya mwezi Mai hadi Juni,
2011.
Kuna ukweli
uliopo juu ya hili. Ndani ya miaka hii mwanamke ujikuta anaingia katika
majaribu yasiyo na msingi huku akijitahidi kutafuta mme mzuri kwake, na matokeo
yake huishia kuchezewa na hatimae kukosa wote. Wanaume ndio wasababishaji
wakubwa wa mke huyu asiolewe au asipendwe. Angalia mfano huu, mti ukichipuza maua utamuona mdudu wa
kila aina akiwemo nyuki, nzi, kipepeo na wengine wemgi wakiingia na kutoka.
Haya ndiyo yaliyopo kwa wanawake kwa kipindi hicho tajwa hapo juu.
Hapa lile neno
langu love is something natural (mapenzi ni kitu cha asili) hutumiwa vibaya na
badala yake mapenzi hupoteza umaana wake. Kwa kila mtu mwenye upendo wa kweli
hawezi kumdarau mchumba au mke/mme wake. Na inapotokea vinginevyo ni makosa ya
kibinadamu ambayo hutokea baina ya hawa wapendanao.
NINI MAANA KUPENDA AU KUPENDWA
Inawezekana si
mara yako ya kwanza kusikia nini kupenda. Haya yamewai kuzungumzwa na msanii wa
muziki Mwijuma Mumini. Neno kupenda lipo katika nyoyo za binadamu na uwezi
kuona kwa macho. Kwa kifupi ni neno la kufikirika tu. Lakini utagundua kweli
unapendwa na kupenda mara baada ya kukutana na mke, mme au mchumba wako.
Matendo ndiyo yanayoonyesha kweli unapendwa au unampenda.
Kwa kawaida mtu
anayetaka kuwa na mahusiano na wewe
huanza kuonyesha kwa sura pamoja na maneno yaliyojaa utamu. Na mara
uyasikiapo maneno hayo ndipo hamu na shauku ya kuendelea kuwa naye inakujia na
hatimaye mwisho wa siku mnaamua kuwa na makubaliano. Kwa kuwa utamaduni wa
baadhi ya jamii katika bara letu la Afrika unamnyima mwanamke kutamka neno
nakupenda kwa mwanaume, basi hapo lugha itayotumika ni ile ya ishara ya kuweza
kumvutia mwanaume kwa kila hali ili awe naye katika ukrasa wa mapenzi.
Na pale mwanamke
anapotamka neno nakupenda “I love you” kwa mwanaume, inaonekana mwanamke yule
ni mmalaya wa hali ya juu. Hii ni tofauti na nchi za Magharibi ikiwemo marekani
ambako mwanamke au mwanaume ana uwezo wa kuomba uhusiano wa kimapenzi. Kwa
Tanzania kulikuwa na neno “USIONE SOO
SEMA NAE”. Hili neno lilikuwa zuri kuwapa utambuzi wanawake wa kiafrika
kuweza kuomba uhusiano wa kimapenzi kwa mwanaume ampendaye na si kutegemea
afuatwe.
Tabasamu zito,
na tabia ya mwanamke huanza kuonyesha kuwa ni bora au mzuri kuliko za wengine.
Lingine ni kwamba maneno ya kumsifu mtarajiwa yanakuwa mengi. Mara umependeza,
mara leo tutoke out (kwenda kupumzika eneo fulani kama
vile maeneo ya starehe au sehemu yeyote waipendayo watarajiwa). Na hapo ndipo
mmoja kati yao huanza kutamka neno linalostahili
ili kuwezesha mahusiano, na kuna wengine hufikia kutamka hata kama
ni siku ya kwanza kuonana/kukutana. Haya ni baadhi tu ya mambo yanaoonyesha
kuwa mtu anapenda au anapendwa kabla ya kuanza mapenzi motomoto.
MWANZO WA MAPENZI
Mapenzi huanza
na moto wa hali ya juu. Kila mmoja anataka na kupenda kukaa wote muda wote.
Kila neno linalozungumzwa na mmoja wao huonekana zuri. Hapo ndipo mke au
mwanaume huamua kutoloka kwao na kumfuata mwenzi wake. Hapa wapendanao hujikuta
kama wapo nchi nyingine. Maneno ya utamu kama
neno nakupenda hutamkwa kwa sana
tena kwa mkazo kwa wakati wote.
Kila mmoja huona
amefika sana.
Na mara nyingi mtu awezi kuamini jambo lolote analoambiwa na mtu mwingine. Haya
yameonekana sana katika Tamthilia zinazopendwa
na vijana wengi kama zile za nchi za
Magharibi. Mfano ni ile iliyogusa nyoyo za watu wengi maalufu kwa jina la “Malichui” au AN ENGEL. Na LOVE TO DEATH.
Penzi hufikia
kileleni na wengine huanza hatua za utambulisho kwa wazazi. Kwa sasa
utambulisho huu hufanya na mototo mwenyewe. Hii ni tofauti na miaka ile ya
nyuma ambapo mme au mke huchaguliwa mke au mme na wazazi wake. Haya ndiyo mambo
ya sasa. Kila kitu uwekwa wazi na wapendanao wenyewe.
Kwa wale
wanaobahatika kuweza kufunga harusi uweza kufunga harusi na wangine huishia
njiani bila mafanikio kutokana na sababu mbalimbali zilizo nje au ndani ya
uwezo wao. Sababu ni nyingi hivyo mwandishi hakuweza kuzitaja zote lakini uk 7
& 8 zinajieleza wazi.
KUTENDWA
Hili ni neno
lililoibukia siku za hivi karibuni na kuonekana kuwa ni umaarufu sana miongoni mwa vijana.
Watu hutumia neno hili wakimaanisha kuachwa na mwenza au mpenzi pasipo
kutarajia kutokana na matendo aliyofanyiwa. Hii ndiyo tafsiri yake. Ni mara
nyingi sana jambo kama
hili limewatokea wapendanao. Wangine husema amemwagwa au amebwagwa chini. Hii
ni misemo ya vijana wetu wa siku hizi. Inawezekana kwa wengi na si wewe tu umewai
kusikia neno hili la kutendwa. Si geni kiasi kwamba mtu anaweza kutoelewa
kinachoozungumzwa.
MAMBO MAKUU YANAYOSABABISHA KUTENGANA KWA WAPENDANAO
- Kutofanya uchaguzi ulio sahii wa mke/mme au mchumba. Vijana wengi siku hizi hujilaumu sana juu ya chaguo la mwenza wake. Ukikosea mwanzo ujue utaoa na kuacha mke zaidi ya mmoja. Pakifikia mahali unaanza kutamani wanawake/mwanaume wa nje na kumsahau wako wa ndani ujue ni ishara kwamba hukufanya chaguo zuri ujana wako.
- Wazazi kutopendezwa na mke/mme. Hapa wazazi nawazungumzia wale wanaopenda kuingilia mambo ya ndani ya watoto wao. Kuna watu wanaitwa mawifi, hawa ndio chokochoko kubwa na mke na mme kutengana. Watatumia maneno ya uzushi na unafiki ili mradi mke au mme yule waachane. Mwisho ndoa au uchumba unavunjika.
- Dini tofauti. Hili ni suala la mdahalo karibu dunia mzima. Inapotokea mme na mke wameanzisha uchumba, na kila mtu ana dini yake, mwanzo wa penzi hakuna aneyekumbuka nini athali kwa hapo baadaye. Muda unasonga, na kila mmoja anahitaji afunge ndoa au wazazi wafahamu, hapa kila mmoja anaanza kukumbuka utofauti wao. Kutokana na imani kali au kutokuwa na uelewa mwanzo, wanaamua kutengana ili kulinda maslahi ya dini au dhehebu la kila mtu. Hii mara nyingi hutokea kama mmoja wao ni Mkristo au Muislam. Katika ndani ya ukristo kuna misingi inayoongoza kanisa la SABATO. Hapa pia hawaruhusu muumini kuoa au kuolewa nje ya dhehebu hili vinginevyo anatengwa na kanisa.
- kutofikia kilele wakati wa tendo la ndoa. Hakuna ndoa inayoweza kudumu kama tendo la ndoa halifanyiki. Au kama linafanyika ni kwa kulidhika mmoja na mwingine asitosheke. Hii ni sahemu muhimu sana inayomfanya mke au mme aweze kuwa na mahusino na mtu mwingine ili aweze kujitosheleza. Kila mmoja hupenda atosheke, na inapotokea vinginevyo migogoro huanzia hapo na hatimae kuvunjika kwa penzi lao. Zao la hili ni kutoroka kwa mke/mme au mchumba na kuanzisha uhusiano na mtu mwingine.
- Tabia ya uzinzi kupindukia. Hapa nazungumzia tabia ya umalaya ya mwanamke au mwanaume nje ya mpenzi wake. Hawa ni watu ambao uzaliwa na genes za aina hiyo na wamerithi kutooka kwa wazazi. Hivyo kwa mtu aliyorithi inakuwa ni rahisi zaidi kutoka nje ya ndoa yake na kwenda kufuata wengine ili mradi atimize malengo yake. NB. Tumetoa njia za kutatua hili katika kitabu hiki.
- Maneno au mawasiliano. Namna mke na mme wanavyozidisha mawasiliano, ndivyo wanovyoongeza penzi lao. Kwa zamani barua zilikuwa ndio chombo cha mawasiliano kama mmoja wao aliishi mbali. Lakini kwa sasa ni njia ya simu za mkononi. Inapotekea mawasiliano yanapungua kati ya mme na mke kinachofuata ni kusauliana. Kila mmoja atapata wazo la kuwa na mwingine na hatimaye kuanzisha mahusiano mapya na yule ambaye hakupenda kuwa naye. Usipokuwa makini juu ya hili lazima mutatengana tu.
- Wivu. Hakuna penzi linaloweza kudumu kama hakuna wivu. Na wivu huo uwe wa kiasi ambacho akiwezi kuathili penzi lao. Kuna watu wana wivu kupindikia. Hili ni tatizo kubwa, na hakuna mtu anayependa afanyiwe wivu kiasi kwamba hadi mtu anakosa uhuru. Pakifikia mahali hapa wapendanao huanza kutoa maneno ya siri kwa jirani na mwishowe kutengana kwa wependanao. Hapa pia inaambatana na hali ya kutokuwa na imani na mwenza wako.
- Kuwa na mahusiano ya hali ya juu na mtu wa jinsia tofauti pamoja na utani. Mtu ukishaolewa, kuoa au kuwa mchumba ni bora zaidi upunguze mahusiaona ya kupindukia na watu wa jinsia nyingine. Hali ya utani unaoambatana na kushikana, kubusiana pamoja na kuelezana maneno ya kimapenzi kwa wale ambao si wapenzi wako husababisha mgogoro na mwenza wako. Vinginevyo ndoa au uchumba ule utaelekea mahali pabaya na mwisho kuvunjika kwa penzi.
- Kusikiliza maneno ya watu. Kuna watu hupenda kuchonganisha wanawake au wanaume wa watu kwa maslai binafsi. Kwa kawaida watu hawa wapo kwa ajili ya kuona mnagombana. Hivyo basi, kusikiliza kwa maneno ya hawa watu inapelekea kubadili kwa mwenendo wa mweza na hatimaye kuwa mwisho wa penzi.
- Ugumba/tasa. Hii ni ile hali ya mmoja kati ya wapendanao kutokuwa na uwezo wa kuzaa. Yaani kwa mwanaume kushindwa kutoa mbegu zinazoweza kusababisha kutungwa kwa mamba, na kwa mwanamke kushindwa pia kutoa mayai yenye uwezo wa kupokea mamba. Hali hii huwaathiri sana wanawake ambapo mke huonekana mzigo mzito katika nyumba. Wangine wanafikia mahali wanawaambia wapenzi wao kuwa wanajaza choo tu. Hii kauli lazima ipigwe vita sana. Madhara ya kauli zinazofanana na hizo, yule mwenye kizazi huamua kumwacha yule asiye na kizazi na kwenda kufungua kizazi kipya na mtu mwingine.
Hizo ni baadhi ya sababu za kimsingi zinazochangia uvunjifu wa ndoa au
uchumba. Ukweli ni kwamba sababu zipo nyingi lakini zinazoumiza sana vichwa vya watu ni
hizi.Hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini juu ya mambo haya yaletayo mzozo
katika penzi husika.
NAMNA YA KUTATUA NA KUEPUKANA NA MAMBO YAWEZAYO KUSABABISHA KUTENGANA
Kufanya uchaguzi sahihi wa mchumba.
Kila mtu anashauriwa kuchagua mchumba anayekufaa. Si kila mwanamke au mwanaume
ni mzuri kwako na kuanza maisha kama wanandoa.
Jaribu kutafakari na kupata ushauri wa watu walio karibu naye ili upate juu ya
tabia aliyonayo. Ukiona ni mzuri unaweza kuanza hatua za kufunga harusi.
Si vizuri
kuparamia mwanaume au mwanamke unayekutana kwenye basi au kwenye mitandao ya
kijamii kama facebook. Kweli watu wanamaneno
matamu na mazuri sana,
lakini walio wengi ni wababaishaji wa mapenzi. Jiulize swali dogo tu, ameonana
na wanaume au wanawake kama wewe wangapi. Jibu
ni wengi, hivyo kuwa mtulivu, siku ikiwadia utampata mzuri zaidi ya huyo
(simahanishi mtengane na mme/mke au mchumba uliyenaye sasa).
Wazazi hawana budi kupewa elimu ya kutosha
juu ya mke/mme au mchumba wako. Mwenye haki ya kuchagua mchumba ni wewe na
sio wazazi wako. Wewe ndiye unayefahamu unampenda kiasi gani. Jaribu kuwashauri
hadi wakuelewe kwa nini unataka kuwa na huyo mchumba wako. Hapa hauna budi
kupunguza hasira kwani wazazi wengine wana tabia ile ya kuhukumu mtu mara tu
baada ya kuanza kuongea naye.
Kama wapendanao hamna budi kuendelea kushirikiana nao kwa
karibu, na mwisho wa siku hali waliyonayo itatoweka na badala yake uhusiano
wenu utaendelea kukua. Usiwatamkie maneno makali wale wote wanaokupinga juu
huyo mchumba wako. Kwa kufanya hivyo uhusiano wenu utadumu maisha milele.
Ni muhimu kuweka makubaliano juu ya dini za
wapendanao. Hili ni jambo linaloumiza sana
vichwa vya watu ulimwenguni. Suala hili ni suala la mdahalo usio na mwisho, na
uhishia tu pale wapendanao wanapoamua kufuata majibu na mapatano yao.Kama
mke/mme wako ni dini tofauti na yako, basi nakushauri muanze kupanga mikakati
pale tu mutapoamua kuanza uhusiano wenu. Mweleze ukweli huyo mchumba wako juu
ya dini yenu na mnavyoishi kule kwenu. Baada ya hilo muendelee kupanga hatima ya kizazi chenu
na athari zipi zitawapata na mutatatua vipi hizo changamoto zote. Changamoto
ambazo huathiri sana
ni hatima ya watoto. Hapa kama msimamo haupo juu ya maamuzi yenu basi tambueni
huo utakuwa mgogoro usio na mwisho. (Hapa nimezungumzia tu kwa wale walio na
wanaotarajia kuingia kwenye uchumba).
Kwa wanandoa kama walifanya maamuzi bila kujijua basi nashauri
waendelee kufuata utaratibu wao na pale inaposhindikana muwaone wataalamu wa
masuala ya mahusiano katika jamii wakiwemo watu wa ustawi wa jamii.
Ni vizuri kumfikisha mwenza wako kileleni.
Wanaume walio wengi hushindwa kuwafikisha wake zao kileleni. Hii yote inatokana
na kushindwa kujua namna gani ya kumwandaa mke au mchumba wake ili afikie
kileleni. Walio wengi wanaamini wakishafikia hatua ya kupezi mara mbili wanaona
wamemfikisha mke kileleni. Nakushauri usome kitabu kilichoandikwa na Dr Paul. Mara
nyingi husikika siku ya jumatano katika RFA (Radio Free Africa) kuanzia saa
tano usiku.
Utajua namna ya
kumfikisha mke wako au mme wako kileleni. Pia kuna wanaume ambao hukosa kufikia
kileleni. Hii husababishwa na mke kutojua namna ya kumfikisha mme kileleni.
Hivyo kupitia kitabu cha Dr Paul Nelson utaweza kujua sehemu zipi zinapaswa
kuguswa ili kumfikisha kileleni. Kitabu kinachozungumzia namna ya kumfikisha
mpenzi wako kinaandaliwa. Kwa wale wapenzi wa facebook munaweza kutembelea
ukrasa wangu wa facebook au Arasachi The Centre of Learning”
Kikiwa tayari
muda wowote utakiona sokoni. Kitakuja na kichwa cha habari kisemacho “unafahamu
namna ya kumwandaa mpenzi wako?”. Kulingana na mwili wa mwanamke ulivyo,
unaweza kufanya tendo la ndoa hata masaa mawili na asifikie kileleni. Mke au
mme akifanya vizuri juu ya hili hawezi kumtamani mme au mke mwingine kwa sababu
utakuwa umemjenga kisaikolojia.
Ni vizuri kujizuia tabia ya umalaya kabla
na baada ya kuanzisha uchumba. Hakuna mwenza anayependa kuona mke/mme wake
anatabia ya umalaya. Wengi huzaliwa nayo na kurithi kutoka kwa wazazi. Na
wengine hujengwa na makundi mchanganyiko katika jamii zikiwemo taasisi za
kufundishia.
Kwa mfano Vyuo
vikuu nchini Kenya au nchi
za Magharibi ni kawaida kuwaona wanafunzi wakishikana sehemu mbalimbali za
miili yao
wakiwa maeneo tofauti tofauti ya shule au chuo chao (hawa ni wanalika “peer
group”).
Muhusika hauna
budi kujizuia kwa kuwa naye karibu yule mpenzi wako. Na inavyotokea unaishi
naye mbali basi mtembeleane wakati wa likizo na kupata muda wa kuongea pamoja.
Pia jiepushe kwenda maeneo ya starehe kama
vile baa na ufukweni ukiwa pekeyako pindi mpenzi wako yuko mbali nawe. Kwa
kufanya hili tabia yako utakuwa umeizuia
na kuiacha kabisa.
Mawasiliano lazima yadumishwe. Mwanzo
wa penzi mawasiliano huwa ni ya hali ya juu kwa sababu kila mmoja anapenda
amjue vizuri mpenzi wake. Hii yote hutokea kwa sababu ya upendo walionao kwa
kila mmoja kwa mwenza wake. Siku zinavyosonga mawasiliano huanza kufifia au
kuongezeka kutegemeana na lugha inayoyumika. Hali ya kufifia mara nyingu
hutokea tu mara baada ya kuanza zoezi zima la mapenzi kwa siku ya kwanza. Baadhi ya wanaume hukosa hamu ya kuendelea
kuwa naye kama mpenzi wake. Lakini baada ya
siku chache mkizidi kuwasiliana hali inarudi kama
kawaida. Hii hutokea sana kwa wanaume, na kama
kwa wanawake ni kwa kiasi kidogo sana.
Hapa ndipo utapoona yule uliyempenda umetengana ghafla.
Mukifikia hatua
hii mnapaswa kuendeleza na mawasiliano. Kwani kitendo cha kutengana ghafla
huwaumiza sana
wanawake kwa sababu inaonekana lengo kubwa ni kumchezea na kumwacha. Ili
kudhibiti hali hii mnatakiwa kudumisha mawasiliano na kuendelea kuwa karibu sana na baada ya wiki moja
hali itarudi na kuwa na hamu ya kuwa na wewe muda wote. Hapo ujue kuwa hali
imeshatoweka na sehemu iliyobaki ni ya kuendelea kujipangia mikakati juu ya
mahusiano yenu ili kudumisha penzi lenu. (hali hii ni kwa baadhi tu ya watu na
hutokea kama mke au mme hakuweza kumfikisha
kileleni mwenza wake. Ni vizuri mfanyie surprise ya ukweli siku ya kwanza ili
asikusahau kamwe maishani mwake. Walio wengi huikumbuka sana yale yaliyotendeka siku ya kwanza
kufungua penzi lao).
HATUA ZA KUJUA PENZI LINAPOTEZA UELEKEO.
Hatua kuu zinazoonyesha penzi limepoteza uelekeo ni hizi hapa:-
1.
MAWASILIANO KUWA DUNI
2.
USO KUONESHA KUWA HAPENDI KUONGEA
3.
HASIRA ZA MARA KWA MARA
4.
MANENO YASIYOFAA HUANZA KUZUNGUMZWA
5.
KUDAI KUTENGANA
1. MAWASILIANO KUWA DUNI
Mapenzi na sawa
na jani la mti. Huendelea kuwa na mawasiliano na shina kwa kusaidiana na
matawi. Ila siku ikifika jani linadondoka. Hii utokea pale jani linapochoka na
maisha ya kujishikiza. Haya ndiyo sawa yalio kwetu binadamu. Mwanzo uanza kwa
kasi zaidi na mwisho hufifia kwa mawasiliano. Mtu anaweza kukata mawasiliano
kwa sababu zake binafsi zikiwemo hizo za hapo juu.
Kama mawasiliano yalikuwa ni mara tano kwa siku (kwa wale
walio mbali, mfano masomoni.), basi mawasiliano yanaaza kushuka hadi mara mbili
hadi mwisho wa siku mawasiliano kukaka kabisa. Hapa kila mmoja akiulizwa swali
kwanini husema nilibanwa na kazi ndio maana sikuweza kukutafuta.
Kwa walio kwenye
ndoa mawasiliano pia yanakuwa nyuma kidogo. Kama
alikuwa anakusalimia kwa kukumbatiana, hapa hali hua tofauti kabisa. Muda
mwingine kila mtu na kazi yake. Kila mtu shuka yake, na kukicha kila mtu
kivyake.
Hii hua na
athari sana
pale mmoja wa wapenzi anapokuwa na mpenzi mwingine. Yule ambaye ulidhani umemchagua
anakuja kuwa sumu kwako. Unapenda umwone yeye ataki. Unapenda umpe zawadi yeye
ataki, unapenda kutoka naye out yeye ataki, na pale anaposema uwasiliane naye
basi roho huweka pembeni. Utagundua kuwa kama
analazimishwa aongee.
Ikifikia sehemu
hii na kama ulimpenda kweli basi utaongeza
jitihada za kutaka kuwa naye, wasio na imani hufikia mahali wanasema
nitaendelea kukaa bila kuoa. Kauli hii ni udanganyifu tu. Akisahau yale
yaliyomtokea, anaamua kusaka mke au mume mwingine. Unapoona hali hii imeanza
jalibu kuwajilazimisha kuwa karibu yake sana.
Na pale unavyoona hali ni mbaya zaidi basi mweleze rafiki yake wa karibu ambaye
humwamini kwa kila jambo.
Au unaweza
kumweleza mtu anayeheshimika ili asikilize kilio chako na mwisho wa siku utaona
mafanikio. Hii ni kwa wachumba na hata kwa wanandoa itapotakiwa kufanya hili.
Kwa wanandoa ni
muhimu wawaone pia wezee wa busara ambao wanaaminika na kukubalika na jamii.
Ikishindikana basi waende katika ofisi ya kata au ustawi wa jamii kwa msaada
zaidi.
2. USO HUONYESHA KUWA HAPENDI KUONGEA
Ni hali ya
kawaida kuona mke au mme kuonyesha kuwa apendi kuongea na wewe. Sababu kubwa
anayo moyoni na hataki kuisema. Uso mara nyingi unakuwa na asili ya mkunjo kwa
wanawake. Na kwa wanaume sura inakuwa na asili na makunyanzi. Hapo ujue kuwa
hali ni mbaya sana.
Hapo hata ukimsesha anaona kama unajisumbua
tuu. Na kama ataamua kusema ni kidogo tu na
mwisho inaedelea kukaa kimwa.
Pia hata majibu
yake uteyaelewa tu. Ni ya unyonge hivi, na sauti ya chini isiyo na mvuto au
ushawishi kwa mwenzake. Pakifikia mahali kama hapa jalibu kumnunulia zawadi
mzuri, kumkisi, kumwambia oooo mpenzi wangu….nakupenda sana…….leo umependeza namna hii….. Kweli mimi
nimechagua mke mzuri au mme mzuri sana……kwani
najivunia sana
kukuona na kuwa na wewe muda wote.
Wakati mwingine
unaweza kwenda kumsaidia kupika, kuosha vyombo na hata kumwambia mkaoge pamoja.
Utaona jinsi anavyoanza kubadilika mpenzi wako. Hapa hakuna mchawi bali ni
namna tabia yako ulivyomwonyesha. Hali hii haiwezi kwisha ghafla kama kimbunga bali huenda taratibu na mwisho wa siki hali
inajirudia. Kwa hali ya kawaida uchukua kuanzia siku 21-22. Uendelea kumwambia
maneno yenye baraka na busara bila ya kukata tama. Uwe na imanii ya hali ya juu
kwani majibu utayokutana nayo si ya kawaida, lakini mwisho wa siku hali itarudi
kuwa ya kawaida kabisa.
3. HASIRA ZA MARA KWA MARA.
Hatua hii mpenzi
wako huanza kuchukia kila jambo. Utende mema yeye kwake ni baya. Utajiongelesha
ni kama unamuongezea hasira. Hapa ndipo watu
huwa wanafikia kuchukua hatua ya kujiua wenyewe kisa mpenzi wake amamsaliti.
Mfano wa majibu utayokutana nayo ni kama
haya:-
- mbona hivi mpenzi?
- mimi nifanyaje?
Wewe
yanakuhusu nini?
Umepata
hasara gani mimi kufanya hivi?
Fanya
utakavyo?
Mimi
ndo kila kitu?
- kwa nini yamefikia hapo?
- we ujui?
Hizi ni baadhi
ya changamoto utazokutana nazo wakati wa maojiano yako na mpenzi wako. Usimpige
kisa majibu ya mkato. Kama mwanaume hali
ikizidi kuwa ni kelele tu, basi kaa kimya au ondoka na kwenda kufanya shughuli
zingine. Utavyorudi atashindwa anzie wapi.
Kama ni upande wa mwanamke yanamtokea haya basi fanya
hivi:- kaa kimya kwa muda, atakaa kimya mpenzi wako. Kasha usisite kumwandalia
mmeo chakula cha kutosha na kizuri. Hata kama hali usichoke kuandaa. Mpe maneno
matamu mkiwa kitandani na kujaribu kumgusagusa sehemu mbalimbali za mwili. Hapa
mwanaume ujanja unaisha hapo.
Kama hizo njia zinachukuwa muda mrefu basi anza kwa
kumuomba msamaha. Hata kumpigia magoti usione aibu. Piga huku ukionyeshwa kuwa
hali hile upendezwi nayo. Ni ya bahati mbaya. Hakirudi katika hali ya kawaida
na siku nyingi kupita anza kushusha makombola kwa njia ya utani kuwa pale mme
wangu kosa lilikuwa lako. Kama muelewa ataweza kijirekebisha ipasavyo na mwisho
wa siku mukarudi kama siku ya kwanza kuanza
penzi lenu.
4. MANENO YASIYOFAA HUANZA KUZUNGUMZWA
Hii ni hatua ya
nne ambayo inahitaji uvumilivu wa hali ya juu. Mpenzi wako hutamuona mchungu
kupita kiasi. Hutaona kama kuna watu wanamfundisha kuongea maneno haya. Ukweli
ni kwamba ukishaona mke wako mara nyingi yeye na wenzake, hana muda wa kukaa
akuandalie chakula (kwa mwanamke aliye kwenye ndoa) basi ujue kwamba rafiki
zake wamemfundisha na ujue kuna jambo linaendelea ambolo mwisho wake ni
kutengana.
Kwa mchumba basi
utaona maneno ya ovyo ovyo ili mradi umwambie sasa mimi na wewe basi. Atafanya
kila aina awezavyo utengane. Hii huweza kuwa mwanaumme ndio kisa au mke
mwenyewe ndio kisa. Akishindwa hapa anaamua kuchukuwa maamuzi magumu sana ambayo hutasahau tena
maishani. Kama vile kumpigia mpenzi wake mpya
na kuanza kuongea naye.
Hiyo atakuwa
amekuheshimu, anamkumbatia na kumkiss ili mradi uhuzunike kwa hili kasha mtenge
ili awe huru. Hali hii huwa ni mbaya zaidi kama
mtu umependa. Hhiki ni sawa na wanavyofanya wanaume walio wengi katika uchumba
na doa. Ukimuuliza namba hii uliyosevu Juma mbona inaonyesha ni hile ya Asha
atakuambia ni rafiki yangu.
Ukiendelea
kumbana atakuambia ni ya mke wangu. Sasa wewe unasemaje au unataka nini? Haya
utokea kwa wote wenye ndoa zao na wale walio kwenye uchumba bila kujali mme au
mke au mchumba.Haya ndiyo yanayojili sehemu hii iwapo utashindwa kutatua hizo
hatua tatu za mwanzo.
Namna ya kutatua
sehemu hii ni kutumia zile njia elekezi ya hatua ya kwanza. Kubwa zaidi hapa ni
kuomba msamaha kwa kile kinachovumilika, na kile ambacho akivumiliki ni kwenda
kwa washauri nasaha kama vile maafisa ustawi
wa jamii kwa manufaa ya wote. Wao watakusaidia vizuri hata kama
uko peke yako na mwenza wako alikataa kwenda huko. Utamsahau na kuiona dunia ni
tamu zaidi y asana na utasema mwenyewe ulichelewa wapi kipindi yanatokea haya.
5. KUDAI KUTENGANA
Kama mnavyojua, mti uota, ukua, utengeneza majani, huishi
na hatimae mwisho kufa. Hapa mpenzi wako utaona ni balaa tupu. Yaani hafai hata
kidogo. Kama una imani ndogo utatamani uondoke
uende mbali ambako hutamwona tena. Hapa hakuna jinsi, hata mahakama huamua
kutenganisha ndoa kama walioana. Hapa
usipofanya kama atakavyo mpenzi wako unaweza
kuishia hata gerezani au kuchukua uamuzi wa kumpiga.
Kweli inauma sana kumwona mke/mme au mchumba
unaempendaanataka mutengane. Wengine huamua kujinyonga, wengine kunywa sumu,
wengine wanaamia baa na kuweka makazi yao.
Mmoja hakikataa hakuna jinsi, mwache aende kwa usalama.
Jinsi ya kutatua
hili ni kwamba unapaswa kwenda kukubali tatizo lililotokea. Kwani kinachotokea
kwa wenzako hata wewe ipo siku yatatokea. Katika maisha ya binadamu kuna
kupenda na kutendwa, hivyo kutengana ni moja ya sehemu ya maisha. Jaribu
kutembelea sehemu zenye mkusanyiko wa watu. Lakini usinywe pombe, na kama ulikuwa unakunya unaweza kuacha kabisa hatakwa miezi
kadha na usitembelee sehemu za pombe.
Unaweza kwenda
disco na sehemu nyinginezo mzuri kama vile
kwenye mpira, kucheza puru, drafti, bao na hata karata. Hali yako itarudi kama zamani. Utajiona wa kawaida (hii ni kama kwa mwanaume). Ukikutana naye usimwone kama ni adui ako mkubwa, kwani yaliyotokea ni majaribu ya
dunia. Na pale mkaapo kwa muda mrefu na kuona kuna umuhimu wa kurudiana basi
murudiane kwa moya mmoja.
Kwa wanawake
huchukua muda mrefu kama tendo lilifanywa na
mwanaume. Na tatizo lenyewe kama kumfumania
mme au mchumba wake wakiwa katika chumba kile kile anacholala yeye. Huwa anaona
ni unyama. Kwa hili, mke huyu kurudiana naye itachukua muda mwingi kwani lile
swala humrudia mara kwa mara. Na kama alimpenda sana bwana wake huamua usikuone kamwe.
Lakini hakuna
jambo lisilo na mwisho. Mme unapaswa kwenda kuomba msamaha kwa yule mke wako
uliyemwacha. Kukataliwa kwa mara ya kwanza ni jambo la kawaida, kwani ile icha
itaendelea kumrudia. Jifanye kama usikii, fanya hivi zaidi ya mara tano hadi
kumi. Mke wako au mme wako ataanza kukuonea huruma na hatimae kuwa naye pamoja.
NB: ieleweke
kwamba si kila unayemfanyia tukio baya ataweza kukusamehe. Ni wachache wenye
nyoyo kama hizo. Bora ubadilike na kutunza utu
na uthamani wako mapema. Kwa kufanya hili maisha utayaona kama
maji ya kunywa.
NANI HUANZA KUMWACHA MWENZAKE KATI YA MKE AU MME
Kuhusu nani
anayepaswa kumwacha mwezake lipo katika sehemu mbili ambazo ni:-
A/ kwa wanandoa
Katika zama hizi
za utandawazi anayepaswa kumwacha mwenzake ni yeyote kati ya mke au mme chini
ya ushahidi na usimamizi wa mahakama. Kila mmoja anayo haki hiyo.
Kinachofanyika ni kwamba mhusika apitie hatua zote za kuachana au kuvunja ndoa yao.
B/ kwa wachumba
Hapa ndipo
inapoanzia balaa. Kila mmoja anataka aanze mwenzake ili apate ya kusema.
Mwanamke anafanya vituko ili mchumba wake aseme basi kuanzia leo mimi si
mchumba wako. Na mwanaume naye husubili kutoka kwa kwanamke aseme mimi basi.
Hapa ni usanii mtupu kwa sababu hakuna anayezifahamu ndoa hizi zaidi ya
marafiki. Na ikifikiwa kujua wazazi basi ujue muda umekwenda sana.
Nilichogundua ni
kwamba, hawa wachumba utengana tu pale anapopata mchumba mwingine anayeridhika
naye. Kuna baadhi wanakuwa na wachumba kwa ajili ya kupeleka siku ili ziende.
Na mwingine anakuwa amejitoa mhanga katika hili. Kwa mchumba asiyehitaji kuwa
na wewe dalili ni zile zile na ndio hatua zenyewe za kuvunjika kwa uhusiano.
Hapa kuna ndoa
za siku moja yaani usiku wanapatana asubihi kila mtu kivyake. Mtu huyu mbinu
anayoingia nayo ni ya kumwonea huruma sana,
lakini saa chache tu baadaye hali ni mbaya. Kila ukimgusa mchungu kama pilipili.
Kuna ule uchumba
wa muda mrefu. Ambao watu hukaa zaidi ya miezi mitatu. Hapa wapendanao huachana
kwa ugomvi au kupata kwa mke au mme mwingine ambaye anaonekana anamfaa.
HALI BAADA YA KUTENGANA
Kwa walio wengi
hapa hali hubadilika na kuwa tofauti na mwanzo. Lakini ukweli ni kwamba hutokea
hali za aina kuu mbili ambazo ni hali ya maelewano na hali ya kutoelewana.
A/ Hali ya
kutoelewana
Hapa kama
wapenzi hawakubahatika kuwa na mtoto basi kila mtu huanza kumchukia mwenzake na
kufikia hatua ile hata kuto salimiana. Ieleweke kuwa hii ni kwa baadhi ya watu
tu. Na kama mlikuwa na watoto basi mawasiliano hukata kwa muda mfupi na baada
ya kupita siku kadhaa huanza kuwasiliana kama
mwanzo ijapokuwa kila mmoja hapendi iwe hivyo. Hii hutokea kwa sababu kila
binadamu ana kichaa. Na kichaa uweza kuondoka na hali ikarudi kama
ya zamani.
Kipindi hiki
mwenza wako yupotayari hata kukuondoa duniani, na kwa kuwa sheria humbana,
hutamani kwenda mbali sana
ili mradi asikuone au msionane. Maisha huendelea, na kama
hatatokea mtu ambaye anaweza kumweka sawa (counceling) busi hutokea ile hali ya
chuki juu ya jinsia fulani.
Kama alikuwa ni wa ofisini basi utaona mambo yanageuka na
kuanza kuwa mkali kwa ile jinsia tofauti. Hapa kama ni mwajili mkuu basi
anauwezo hata wa kukukaripia kama motto au
kukufukuza kazi kabisa ndani ya masaa 24.
Ushauri wangu ni
kwamba, ukiona hali hii imeanz kutokea kwa mfanyakazi mwenzako au mwajiliwa
mwenzako, au yule mpenzi uliyemwacha na hata ndugu yako, naomba uwe naye karibu
sana hata kama
maneno unayopewa ni ya kukatisha tama. Endelea kumsaidia kazi ndogo ndogo,
kufanya mazoezi ya viongo, kutembelea maeneo mbaalimbali na kumshauri
mutembelee zile ofisi za ushauri nasaha kwa ajili ya kuweza kumrudisha hali
yake kuwa ya kawaida.
Inachukuwa muda
mrefu sana
kukubaliana na wewe kuwa mpenzi wako aua rafiki yako mpendwa au hata ndugu yako
kukuelewa kuwa ana tatizo. Hapa hujikuta kila jambo analofanya na kuamua liko
sahihi. Usikate tama juu ya majibu unayopewa. Yatumie majibu hayo kama changamoto kwako. Mtu ambaye huweza kumsikiliza mtu
wa namna hii ni yule tu aliye karibu naye tu.
Hali hiyo huweza
kutoweka mapema kutegemea na wale walionae karibu wanavyomshauri mlengwa.
Ikumbukwe kwamba si kila rafiki ana maneno ya busara kwako. Huyo rafiki yako
ndiye mbaya wako wa kesho. Leo anakupenda na kesho anakugeuka. Na si kila
rafiki ni mbaya kwako. Unatakiwa kuangalia rafiki yupi ni bora zaidi na
anayekufaa ili akusaidie wakati wa shida badala ya kukuangamiza.
B/ Hali ya
maelewano
Hapa wapendanao
huendelea kuwasiliana vizuri kama kipindi cha
penzi lao. Hali inakuwa tofauti kidogo lakini mawasiliano ni mazuri. Hii
hutokea pale mke au mme au mchumba wameachana kwa njia ya amani.
ATHARI ZA KUPENDA KUPITA KIASI
Ni vyema kujua
mpenzi wako anakupenda kiasi gani. Na kila mtu ni siri yake mwenyewe kujua
anampenda mwenzi wake kwa kiasi gani. Kumpenda mke au mme au mchumba wako ni
jambo jema sana.
Muonyesheshe namna upendavyo kwa maneno, pamoja na tabia yako.
Kuna jambo moja
ambalo mtu yeyote apendezwi nalo kuona mme, mke au mchumba akilitenda ambalo ni
kuonyesha dharau ikiwemo kuona maneno anayozungumza hayana mantiki yeyote.
Akigundua mwezi wako ujue kuwa hali ya penzi lenu linaelekea kubaya. Si vizuri kuendekeza hali
hii kama umezaliwa nayo au kurithi kutoka kwa
wazazi. Inapaswa ujizuie.
Hakuna mapenzi
ya kweli kama hakuna upendo. Katika maisha ya
sasa ni muhimu sana
kuonyesha namna unavyompenda mke/mme wako. Watu hupenda sana kiasi kwamba hata kufikiri suala
lingine, badala yake huitaji kukaa muda wote na kumfuata kila aendako. Na
wengine ufikia mahali hadi anaharibu kazi. Kila kazi anafanya ili mradi
aonekane amefanya kazi.
Kwa kawaida
imezoeleka kuona mke au mwanamke ndiyo anayependa sana kuliko mme wake. Kiukweli ni kwamba wote
wana haki ya kuonyesha kila aina ya upendo alionao kwa mweza wake.
Zifuatazo ni
athari za kupenda kupita kiasi kwa wapenzi:-
-Kushindwa
kutekeleza majukumu ya kila siku ikiwemo ya kiofisi kwa wafanyakazi.
-Siku ya
kutendwa ikiwadia basi kwa aliyetendwa ni rahisi kupata mshtuko wa moyo
(stress) au kujiua.
-Kutosalimiana
kwa muda mrefu.
-Kushindwa
kusaidiana kwa namna moja au nyingine hasa yale yaliyo nje ya mpaka.
Nadhani
umejifunza mengi sana
katika kitabu hiki. Ni jukumu lako kubadilika na kuwa katika mstari mnyoofu. Mpende
mke/mme au mchumba wako lakini usipitilize kiwango kiasi kwamba unapoteza
welekeo wa maisha yako. Utaumia na kushindwa kufanya maamuzi yako kwa wakati
husika.
Maoni yenu ni muhimu sana
kwangu. Unaweza kutuma kwa anuani zifuatazo:-.
MAWASILIANO
facebook account-
twitter account-
mlawa the center of Learning, on facebook
Phone No.
Kazi hii imeandaliwa na
MLAWA S.S (2014)
VET
Comments
Post a Comment