UVIVU WAKO NI SABABU YA MWENZIO KUCHEPUKA


Mpenzi msomaji, wiki iliyopita nilielezea  kuhusu wanaume wasivyowaelewa wenza wao wanapowaambia wamechoka wanapohitaji kuwa nao faragha.  Kwa nini? Endelea  na darasa hili...
Utafiti unaeleza kuwa wanaume wengi huwa hawakubali neno “nimechoka” ambalo anaweza kuambiwa na mwenzi wake
.
Inaelezwa kuwa asilimia kubwa ya wanawake walio kwenye ndoa ambao walijaribu kueleza hisia zao kwa ‘mamista’ wao kuwa hawapo tayari kwa tendo, walibakwa.Inawezekana hili likawa halipati kujadiliwa sana kwa sababu hadi leo kuna wanawake bado wanaamini kubakwa na waume zao ni sawa. Kinachowapa unyonge huo ni imani kwamba mwanaume ana haki zote za kimsingi za kuutawala mwili wa mwanamke. Ziangalieni nyumba nje ya kuta, ndani kuna mengi!
Ni vizuri kujitambua. Mfumo wa kubakana haukubaliki! Watu waelewe kuwa ni kosa kubwa kubana unyumba, kwani wengi wao wamejikuta wakisalitiwa kwa sababu hiyo. Yapo mambo ambayo natakiwa nikuchambulie ili kufahamu thamani ya tendo ili uelewe tofauti ya chumvi na sukari.
Mapenzi ni tendo la furaha. Wakati wa utekelezaji huwa ni sherehe tupu endapo wahusika watakuwa wamekubaliana kwa moyo mmoja. Yaani hisia zao ndizo zilizowashawishi kuingia kwenye ‘bwawa spesho’. Kinyume chake ni mateso na ndiyo chimbuko la tuhuma za wanandoa kubakana.
“Mwanamke akiolewa haruhusiwi kulala na ‘kufuli’!” Ni msemo ambao unavuma mno. Kinachotajwa hapo ni kuwa anayekubali kuolewa, moja ya masharti ni kukubali ombi la mwenzi wake wakati wowote. Ni kweli? Usiku amelala, ghafla anashtuka uzito umeongezeka kifuani, kuangalia, kumbe ni mume anatimiza haja zake!
Hiyo ni sahihi? La hasha, mapenzi hayapo hivyo! Nimesema kuwa tendo la ndoa linahitaji uhuru wa hisia. Kulazimisha ni kumuumiza. Kukwea juu ya mwenzako bila taarifa ni unyanyasaji. Kila mtu ana wajibu wa kuheshimu mwili wa mwenzake na azitangatie ‘utayari’.
Ni vizuri kujitambua. Mfumo wa kubakana haukubaliki! Ila ni vema pia watu wakaelewa kuwa ni kosa kubwa kubana unyumba, kwani wengi wao wamejikuta wakisalitiwa kwa sababu hiyo. Yapo mambo ambayo natakiwa nikuchambulie ili kufahamu thamani ya tendo!
UTAPOTEZA MVUTO WAKO
Tendo ni chachandu! Kwa wanandoa au wapenzi ambao wanaliheshimu hili na kulitekeleza kwa kiwango bora, huwafanya wenzi wao wawe na hisia za karibu kila wanapowafikiria. Hii ina maana ya kuongeza mvuto!
Mtu ambaye anakuwa mvivu kutekeleza, mwisho wa siku hupoteza mvuto wake. Kwa asili kila binadamu huwa hapendi usumbufu. Alihitaji penzi la amani, ndiyo maana akawa na wewe, lakini kwa kitendo chako cha kutotaka ‘kachumbari ilike’, maana yake unampa mateso aliyoyakimbia.
Anakuomba leo, unamjibu umechoka, kesho tena unaweka ngumu! Hasara kwako hapo ni kupoteza mvuto wa kimapenzi, kwa maana atakapohisi kuhitaji tendo, kila akikufikiria, ataona wewe ni mtata na hueleweki, kwamba akikuomba utamtolea nje.
Itaendelea wiki ijayo.

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU

NINI MAANA YA MAPENZI