Pamoja na hali mbaya uwanjani – Man United wavunja rekodi ya mapato
Manchester
United imeripoti taarifa ya kuongezeka kwa mapato ya klabu hiyo kwa
11.6% kwa awamu ya pili ya mwaka wa kifedha wa klabu hiyo.
Mabingwa haowa Barclays Premier League wamesema mapato yao yameongezeka kutokana ukuaji wa biashara yao ya matangazo na kuuza haki za matangazo ya TV ya kuonyesha mechi zao.
Mapato ya kuanzia kipindi cha October–December yamekuwa mpaka kufikia kiasi cha £122.9m.
Matangazo ya kibiashara yaliongezeka kwa asilimia 18.8%, wakati biashara ya kuuza haki za matangazo ya TV kwa ajili ya mechi zao yalipanda kwa asilimia 18.7%.
Klabu hiyo ilifanikiwa kupata udhamini wa makumpuni sita ya kibiashara.
CEO wa klabu hiyo Ed Woodward alisema kwenye taarifa rasmi: ”Kwa mara nyingine tena tumeweka rekodi ya kuingiza mapato makubwa kutokana na mchango mkubwa tunaopata kutoka washirika wetu wa kibiashara, hali hii inakuja pamoja na kuwa hatufanyi vizuri sana uwanjani, ukiangali nafasi tunayoshika uwanjani, ni jambo la kusikitisha na kila mmoja wetu anajua hilo.”
United kwa sasa wanashika nafasi 7 kwenye ligi na wanaweza kukosa nafasi ya kushiriki kwenye Champions League kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1995
Comments
Post a Comment