BASI LA MTEI LATEKETEZWA KWA MOTO BAADA YA KUGONGA NA KUUA SINGIDA
Habari ambazo mtandao huu umezipata kutoka Singida zinasema Basi la abiria la Matei linalofanya safari zake kutoka Mwanza kwenda Dar limechomwa moto na kuteketea kabisa na watu wenye hasira kali baada ya kugonda bodaboda ambayo ilikuwa imepakia ‘mshikaki’ wa watu watatu ambao walikufa papohapo eneo la tukio.
Hakuna abiria wa basi aliyeumia. Mwandishi wetu aliye kwenye tukio amesema Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela yupo eneo ya tukio akishughulikia sakata hilo.
Comments
Post a Comment