NISHA: MUZIKI NILIFUATA MKUMBO, NAJUTA


STAA wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amesema kuwa katika maisha yake hakuwahi kufikiria kujihusisha na masuala ya muziki, isipokuwa aliingia katika fani hiyo kwa kufuata mkumbo.
Akipiga stori na paparazi wetu, Nisha  alisema imekuwa ni aibu kubwa kujikita kwenye fani hiyo na kukaa
kimya kwa kipindi kirefu kwa kuwa hana mapenzi ya dhati na fani hiyo kama ilivyo kwenye filamu.
“Niliona waigizaji wanaingia kuimba na mimi nikaingia, nilivamia fani tu ndiyo maana  najuta, nimeamua nikae chonjo kwanza na mambo hayo nijikite zangu kwenye filamu,” alisema Nisha.

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU

NINI MAANA YA MAPENZI