Ulimboka, Costa na Pawasa wachambua uchezaji Simba
WACHEZAJI waliojijengea heshima kubwa wakati wakiichezea Simba wametamka maneno ya moyoni kuhusiana na mwenendo wa timu hiyo.
Wachezaji hao ni Boniface
Pawasa, Victor Costa, Selemani Matola na Ulimboka Mwakingwe lakini kocha
Talib Hilal alipowasikia naye akaongeza neno.
Pawasa ambaye alikuwa beki
kisiki alisema: “Kikosi bado kinahitaji kurekebishwa hasa kwenye
kombinesheni ya mabeki na ushambuliaji bado hapako sawa sana. Nafikiri
baada ya mwaka Simba wanaweza kuwa kwenye ubora, wakizingatia misingi ya
usajili, watu muhimu wakae sehemu muhimu.”
Victor Costa ambaye pia ni beki
alisema: “Simba ya..
sasa si ya kutegemea sana kuleta mafanikio makubwa labda siku za mbele mafanikio yataonekana. Wachezaji wanahitaji muda na kuvumiliwa sana. Waachwe makocha wafanye kazi zao na pia wachezaji waliosajiliwa wapewe muda na si kuwafukuza.”
sasa si ya kutegemea sana kuleta mafanikio makubwa labda siku za mbele mafanikio yataonekana. Wachezaji wanahitaji muda na kuvumiliwa sana. Waachwe makocha wafanye kazi zao na pia wachezaji waliosajiliwa wapewe muda na si kuwafukuza.”
Kiungo Selemani Matola alisema:
“Kikosi cha sasa ni kizuri, tena kina vijana vizuri ingawa wanahitaji
kuaminiwa, watachezea timu hiyo kwa muda mrefu kwa kuwa bado ni vijana
wadogo.”
Winga matata Ulimboka Mwakingwe
alisema: “Sasa si kama zamani, wachezaji wengi wa sasa hawajitambui,
hakuna ushindani wowote tofauti na wakati wetu tukicheza kwa kujituma na
kushindania namba.
“Viongozi hawaelewi majukumu yao
wengine wamekuwa wakifanya kazi ya kutafuta wachezaji wa kusajili na
kuishia kusajili wasiofaa kwa kuwa hawana uelewa wa soka.
“Wamekuwa wakijipeleka nje ya
nchi na kusajili vibaya, kisha wanaigharimu timu mamilioni ya fedha.
Majukumu ya usajili wapewe wachezaji wa zamani kutokana na uzoefu wao,”
alisisitiza Mwakingwe.
Kocha wa zamani Talib Hilal aliongeza: “Wachezaji wanatakiwa kujituma na kujiamini zaidi.”
Comments
Post a Comment