JITAMBUE:UHUSIANO KATI YA MAPENZI NA HOFU.
SAYANSI ya mapenzi inakataa kuwepo mapenzi ya kweli sambamba na hofu. Mtu hawezi kusema anampenda mwenzake wakati kuna vitu anaviogopa kutoka kwa mpenzi wake kiasi cha kumuondolea ujasiri.
Ifahamike kwamba, ukamilifu wa mapenzi kwa ni namna hofu inavyoweza kushughulikiwa na kuondoshwa kabisa miongoni mwa wapendanao.
Uchunguzi unaonyesha kwamba, woga umekuwa sumu kubwa ya mapenzi na mara nyingi imebainika kwamba, kila woga unavyozidi kumwingia mtu ndivyo anavyopoteza mshawasha wa kupenda.
Tunafahamu ubora wa majiko ya gesi lakini wengi wamekuwa hawataki kuyatumia kwa sababu wanaogopa kulipukiwa, hivyo kuamua bora watumie kuni, mkaa au mafuta ya taa ambayo wanaamini ni salama.
Hii ina maana kwamba, mwanamke au mwanaume anaweza kuwa tayari...
kuishi na mtu anayeonekana dhaifu kwenye jamii maadamu hamhofii katika usalama au ustaarabu wa maisha yake.
Kwa msingi huo, hata kama msichana atakuwa mzuri kwa kiasi gani, hawezi kupata mpenzi wa kweli ikiwa atakuwa mtegeneza hofu miongoni mwa wavulana anaokutana nao. Akitoa nafasi ya kuogopwa na wanaume kwa ukali, majivuno huku akiwatia hofu ya kuwasaliti kwa uzuri wake na pengine wasijiamini kifikra atajikuta akihangaika sana kumpata mpenzi wa kweli.
Mada hii inalenga kueleza jambo moja muhimu nalo ni kuhakikisha maisha ya mapenzi yanakuwa salama, hayana woga wa kusalitiana, kutengana, kutosikilizana, kuhujumiana, kuambukizana magonjwa ya zinaa na hata woga wa kutosikilizwa.
Mwanamuziki 2pac alisema katika moja ya mashairi yake kwamba, Fear is stronger than love, akimaanisha woga una nguvu kuliko mapenzi.
Ikumbukwe, vitisho kwenye mapenzi viko vingi, wakati mwingine msichana anaweza kutishika na utajiri au umaarufu wa mumewe kiasi cha kuona hayuko salama kimaisha.
“Aaa mimi sijui kama tutadumu si ujajua mwenzangu tajiri/maarufu wengi wanamtaka.” Hali hii ikiwepo moyoni kwa msichana bila kuondolewa, kiwango chake cha kupenda kitapungua.
Hebu jiulize ulimwengu wako wa mapenzi na huyo umpendaye umeujenga kwenye misingi gani, uko huru au unaogopa mambo na matendo fulani ya mwenzio? Mwambie hofu ina nguvu kuliko mapenzi.
Nashauri kabla hujapambana na mpenzi wako katika jambo lolote unalodhani halitendi kwa usawa, shughulikia hofu yako na uiondoe kwanza. Wakati mwingine unaweza kuwa mtu wa vurugu si kwa sababu mume/mkeo ana matatizo bali ni hisia zako za kusalitiwa, kuachwa au kudhulumiwa mali ndizo zinazokutesa.
Comments
Post a Comment