Watu watano wakamatwa
Polisi nchini Tanzania wamesema
shehena ya Pembe za Tembo zilizokamatwa katika bandari ya Zanzibar ni
sawa na Tembo mia tatu na watano, zikiwa na thamani ya karibu shilingi
bilioni nane, sawa na karibu dola milioni tano za Kimarekani.
Watu wawili wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma
za kuhusika na pembe hizo, huku maafisa wawili wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania, TRA, na mmoja wa Mamlaka ya Bandari pia wamekamatwa kuhusiana
na tukio hilo.Pembe hizo zilikuwa zimefichwa kwenye kontena la urefu wa mita 40, tayari kwa kusafirishwa kwenda nje ya nchi.
Serikali ya Tanzania iko katika kampeni kamambe ya kupambana na ujangili ili kunusuru wanyama pori ambao wako hatari kutoweka kutoka na kushamiri kwa biashara ya meno ya tembo na vipusa vya faru.
Iliripotiwa kuwa wastani wa tembo 30 huuawa kila siku nchini Tanzania, hali iliyoilazimisha serikali kukabiliana na mtandao wa ujangili, ambao unatuhumiwa kuunganisha watu wa kada mbalimbali, wakiwemo wawindaji, wasafirishaji na wafanyabiashara wakubwa ndani na nje ya nchi.
Hivi karibuni raia watatu wa China walikamatwa nchini Tanzania kwa kukutwa na pembe 706 ya tembo, sawa na Tembo 353 waliouawa katika hifadhi mbalimbali nchini humo.
Comments
Post a Comment