MSHINDI KUTOKA BIBI BOMBA AMEPATIKANA:
NA JELARD LUCAS(GLP)
MASHINDANO ya kumtafuta Bibi Bomba yalimalizika usiku wa kuamkia leo
katika ukumbi wa Complex uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam na
mwanamama Mgeni Ibrahimu kuibuka kidedea.Kwa kuibuka mshindi, Mgeni alijinyakulia zawadi ya kitita cha shilingi milioni 12 zilizotolewa na Clouds Media Group ambao ndiyo walikuwa waandaaji.
Katika shindano hilo lililohudhuriwa na mke wa Meya wa jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi, aliyemwakilisha Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba, Veronica Kayombo alitwaa nafasi ya pili na kuondoka na shilingi milioni 5 huku nafasi ya tatu ikikamatwa na Thabiza Tungalaja aliyeondoka na kitita cha shilingi milioni 3.
Licha ya kuwazawadia washindi hao watatu wa kwanza, pia washiriki wengine watano waliosalia nao walipewa vyeti na kampuni hiyo kama utambuzi wa ushiriki wao katika shindano hilo la Bibi Bomba Season 2.
Akiongea na Clouds Tv, mshindi wa kwanza, Mgeni alisema amefurahia sana kupokea kwa ushindi huo kwani hakutegemea.
“Nafurahia sana kushinda, nimepokea kwa furaha ushindi huu, sikutegemea kabisa kwani mchakato ulikuwa mgumu,” alisema Mgeni.
Comments
Post a Comment