MONALISA KUFUNGUKA KUPORWA BWANA
http:samwelmlawa.blogspot.comMSANII mkongwe kunako gemu la filamu Bongo, Yvonne Cherry Ngatikwa ‘Monalisa’ amedaiwa kunyang’anywa bwana na shosti wake aliyejulikana kwa jina moja la Doro..
Yvonne Cherry Ngatikwa ‘Monalisa’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Monalisa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi
na mwanaume anayefahamika kwa jina la Yusuph ambapo miezi kadhaa
iliyopita alifanya sherehe ya kuzindua nyumba yake, Kimara jijini Dar
lakini Monalisa hakuhudhuria kutokana na mgogoro uliokuwepo kati yao.Inadaiwa kuwa katika sherehe hiyo, Doro ndiye aliyefungua shampeni. Ikazidi kudaiwa kuwa kuanzia siku hiyo, wawili hao wakawa wapenzi huku Yusuph akionesha mabadiliko makubwa kwa Monalisa. Baadaye aliupata ukweli kwamba wawili hao ni wapenzi.
Chanzo hicho kilisema, Monalisa baada ya kuupata ukweli, aliamua kuachana na Yusuph ili aendelee na Doro.
Waandishi wetu walipomtafuta Monalisa, alikuwa na haya ya kusema: “Wale ni rafiki zangu kama wanapendana sijui, kwanza sipendi kuwaongelea.”
Naye Yusuph alipotafutwa alisema: “Kweli Monalisa ni mtu wangu wa muda mrefu lakini tuligombana kidogo baada ya kupewa maneno ya uongo.” Akafafanua kuwa chanzo cha madai hayo ni baada ya watu kumuona Doro akifungua shampeni kwenye uzinduzi wa nyumba yake.
Doro alipopatikana alisema kuwa Monalisa ni rafiki yake wa muda mrefu na hawezi kugombana naye kwa sababu ya mwanaume.
Comments
Post a Comment