Mahakama yaamua kuhusu jina 'Allah'
Mahakama nchini Malaysia,
imeamua kuwa watu wasio waisilamu wasitumie jina 'Allah' kumaanisha
Mungu katika katika imani zao na kubatilisha uamuzi wa mahakama ndogo
uliotolewa mwaka 2009.
Mahakama ya rufaa ilisema kuwa jina Allah
linapaswa tu kutumiwa na waumini wa kiisilamu la sivyo linaweza kuzua
taharuki miongoni mwa jamii.
Wakristo wanateta kuwa wamekuwa wakitumia jina hilo la Allah katika lugha ya Malay na ambalo lilitokana na lugha ya kiarabu kumaanisha Mungu kwa miaka mingi na kuwa uamuzi wa mahakama unakiuka haki zao.
Mwanamke mmoja mkristo alisema kuwa uamuzi huo utaathiri jamii pakubwa.
"ikiwa tutawazuia watu wengine kutumia jila la Allah, basi itatubidi kutafsiri Bibilia nzima upya" Ester Moiji kutoka jimbo la Sabah aliambia BBC.
Umauzi ulitolewa na mahakama ndogo mwaka 2009 ulisababisha taharuki baina ya waisilamu na wakristo huku makanisa na misikiti ikishambuliwa.
Ilitokea baada ya serikali kusema kuwa jarida la kikatoliki la The Herald, haliwezi kutumia jina Allah katika makala yake ya lugha ya Malay kumaanisha Mungu kwa kikristo.
Wahariri wa jarida hilo lilikwenda mahakani kupinga uamuzi huo na mahakama ikafanya uamuzi uliowapendelea. Serikali baadaye ilikata rufaa.
Lakini katika uamuzi wake leo, jaji alisema kuwa jina Allah haliwezi kutumika kwa dini ya kikrsito kumaanisha Mungu na kuwa ikiwa jina hilo litatumiwa basi huenda likazusha taharuki baina ya jamii.
Mhariri wa jarida hilo alisema kuwa alighadhabishwa na kushangazwa sana na uamuzi wa mahakama na kwamba atakata rufaa.
Wafuasi wa jarida hilo wamesema kuwa Bibilia zilizoandikwa kwa lugha ya Malay zimekuwa zikimtaja Allah kumaanisha Mungu kwa kikristo tangu zamani sana.
Comments
Post a Comment