Arsenal nje ya kombe la Capital One


Juan Mata wa Chelsea akisherekea bao dhidi ya Arsenal
Katika mashindano ya Capital one huko uingereza Arsenal ambao wako kileleni mwa ligi kuu ya uingereza waligaragazwa bila huruma na Chelsea kwa mabao mawili kwa bila. Lakini Chlesea walipokuwa wakiwatesa the Arsenal nyumbani kwao Manchester United waliwachapa Norwich kwa mabao manne kwa bila.
Hii inafanya Man u Kushinda mara sita mfulululizo, bila shaka na kumpa Moyes matumaini ya kufanya vizuri katika ligii ya Uingereza halikadhalika kombe hilo la Capital one
.
Na katika kile kinachonekana kuwa wanasoka wa afrika wameshuka katika chati ni kiungo wa kati Yaya Toure pekee kutoka Ivory Coast ambaye yumo katika orodha ya wachezaji 23 walioteuliwa kuwaniwa tuzo ya mchezaji bora wa Fifa mwaka huo.
Kwa sasa wachezaji nyota wa zamani kama Didier Drogba, Samuel Eto'o na Michael Essien wanaonekana kufifia.
Na Yaya Toure yuko nchini Kenya katika juhudi za kupiga vita biashara haramu ya pembe za ndovu.
Toure saa ni balozi wa shirika la mazingira duniani UNEP. Mchezaji huyo mshidi mara mbili barani Afrika alifurahi katika hotuba yake kukubali wadhifa huo mpya.

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

NINI MAANA YA MAPENZI

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU