SIMBA KILELENI KWA KUONGOZA LIGI KUU..
-SHUJAA SIMBA NI MRUNDI TAMBWE, APIGA 4 MGUUNI!
-MABINGWA YANGA WANASA TENA MBEYA!!
-JUMAMOSI: AZAM FC v YANGA!!
LIGI KUU VODACOM, VPL, imeendelea tena na Simba leo imenguruma Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
Salaam kwa kuitandika Mgambo JKT Bao 6-0 na kukwea kileleni wakiwa
Pointi 1 mbele ya waliokuwa Vinara Ruvu JKT ambao leo wamepigwa 1-0 na
Ruvu Shooting.
Mabingwa Watetezi Yanga leo tena
wametoka Sare ya Bao 1-1 na Prisons huko Mbeya licha ya wao kutangulia
kufunga katika Dakika ya 41 kwa Bao la Jerry Tegete lakini Prisons
wakasawazisha katika Dakika ya 77 kupitia Peter Michael.
MATOKEO:
Septemba 18
Tanzania Prisons 1 Yanga 1
Simba 6 Mgambo JKT 0
Kagera Sugar 1 JKT Oljoro 1
Azam FC 1 Ashanti United 1
Coastal Union 1 Rhino Rangers 1
Mtibwa Sugar 0 Mbeya City 0
Huko Azam Complex, Wenyeji Azam FC
walitoka 1-1 na Ashanti United ambao walisawazisha Bao kwenye Dakika ya
78 Mfungaji akiwa ni Anthony Matangalu.
Bao la Azam FC lilifungwa na Kipre Tchetche katika Dakika ya 20.
Kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
Salaam, Simba waliibuka na ushindi wa Bao 6-0 dhidi ya Mgambo JKT na
kutwaa uongozi wa Ligi wakiwa na Pointi 10 wakifuatiwa na Ruvu JKT wenye
Pointi 9 ambao wako sawa kwa Pointi na Ruvu Shooting.
Kwa Sare ya leo, Yanga wapo nafasi ya 4 wakiwa Pointi 3 nyuma ya Vinara Simba.
Shujaa wa Simba kwenye ushindi wao mnono
wa leo ni Mchezaji kutoka Burundi, Amisi Tambwe, aliepiga Bao 4 huku
nyingine zikifungwa na Kijana mdogo Haroun Chanongo.
RATIBA:
Jumamosi Septemba 21
Mgambo JKT v Rhino Rangers
Tanzania Prisons v Mtibwa Sugar
JKT Ruvu v JKT Oljoro
Simba v Mbeya City
Azam FC v Yanga
Kagera Sugar v Ashanti United
Coastal Union v Ruvu Shooting
VPL-MSIMAMO:
NA | TIMU | P | W | D | L | GD | GF | POINTI |
1 | Simba SC | 4 | 3 | 1 | 0 | 9 | 11 | 10 |
2 | JKT Ruvu | 4 | 3 | 0 | 1 | 5 | 6 | 9 |
3 | Ruvu Shooting | 4 | 3 | 0 | 1 | 4 | 6 | 9 |
4 | Yanga SC | 4 | 1 | 3 | 0 | 4 | 8 | 6 |
5 | Azam FC | 4 | 1 | 3 | 0 | 2 | 5 | 6 |
6 | Coastal Union | 4 | 1 | 3 | 0 | 2 | 4 | 6 |
7 | Mbeya City | 4 | 1 | 3 | 0 | 1 | 4 | 6 |
8 | Mtibwa Sugar | 4 | 1 | 2 | 1 | -1 | 3 | 5 |
9 | Kagera Sugar | 4 | 0 | 3 | 1 | -1 | 2 | 3 |
10 | Rhino Rangers | 4 | 0 | 3 | 1 | -2 | 4 | 3 |
11 | Mgambo JKT | 4 | 1 | 0 | 3 | -8 | 1 | 3 |
12 | JKT Oljoro | 4 | 0 | 2 | 2 | -3 | 2 | 2 |
13 | Prisons FC | 4 | 0 | 2 | 2 | -6 | 1 | 2 |
14 | Ashanti UTD | 4 | 0 | 1 | 3 | -6 | 2 | 1 |
**MSIMAMO TOKA TFF
VPL: LIGI KUU VODACOM
MATOKEO YOTE:
Jumamosi Septemba 14
Simba 2 Mtibwa Sugar 0
Coastal Union 0 Prisons 0
Ruvu Shootings 1 Mgambo JKT 0
JKT Oljoro 1 Rhino Rangers 1
Mbeya City 1 Yanga 1
Kagera Sugar 1 Azam FC 1
Ashanti United 0 JKT Ruvu 1
-----------
Jumatano Agosti 28
Mtibwa Sugar 1 Kagera Sugar 0
Rhino Rangers 0 Azam FC 2
Mbeya City 2 Ruvu Shootings 1
Mgambo JKT 1 Ashanti United 0
JKT Oljoro 0 Simba 1
Yanga 1 Coastal Union 1
JKT Ruvu 3 Prisons 0
------------
Jumamosi Agosti 24
Yanga 5 Ashanti 1
Mtibwa Sugar 1 Azam FC 1
JKT Oljoro 0 Coastal Union 2
Mgambo JKT 0 JKT Ruvu 2
Mbeya City 0 Kagera Sugar 0
Ruvu Shooting 3 Prisons 0
Rhino Rangers 2 Simba
Comments
Post a Comment