Moyes awaomba subra mashabiki
Kocha wa Manchester United David
Moyes amewaonya mashabiki wa mabingwa wa ligi kuu ya England kwamba
anahitaji kuimarisha kikosi chake na kwamba kipigo cha Jumaapili ambapo
walichapwa 4-1 na Manchester City huenda isiwe ndio mwisho wa matokeo
kama hayo.
"kutatokea siku kama ile ya Jumaapili na huenda
tukakabiliwa na matokeo zaidi kama hayo kwa sababu tuko katika kipindi
cha mpito," alwaaambia waandishi habari kabla ya pambano la Jumaatano la
kombe la Capital One dhidi ya Liverpool...
"tulihitaji wachezaji wawili watatu hivi ambao
wangeweza kuingia moja kwa mopja katika timu. Lakini hayo yatatokea
,kweli huenda itabidi nikabiliane na vipigo vichache zaidi.
Manchester United iliwakosa wachezaji kadhaa
mashuhuri wakati wa kipindi kilichopita cha usajili na hata kulikua na
tetesi za juhudi za dakika ya mwisho za kuipiku Real Madrid ili
kumsajili Gareth Bale ambae kuuzwa kwake kutoka Tottenham Hotspur
kulivunja rekodi kama mchezaji ghali kupita wote duniani.
Juhudi za kuwasajili Cesc Fabregas kutoka
Barcelona, Ander Herrera kutoka Athletic Bilbao na Fabio Coentrao kutoka
Real Madrid ziliambulia patupu.
Leighton Baines aliamua kubaki Everton wakati Thiago Alcantara aliamua kuihama Barcelona na kujiunga na Bayern Munich.
Moyes badala yake alikimbilia kumsajili mchezaji
wa kiungo wa Ubelgiji Marouane Fellaini, kutoka klabu yake ya zamani
Everton, kwa dola millioni ($43.96 ) dakika chache tu kabla ya kufungwa
dirisha la usajili.
Comments
Post a Comment