MOURINHO VICHAPO, MAN UNITED NA NYIMBO, WENGER NA BUTwAA KWA RAMSEY!!
KLABU
Vigogo huko England, Mabingwa Manchester United, Chelsea na Arsenal,
hivi sasa zinapitia kwenye nyakati tofauti huku Stamford Bridge
ikikaribisha vichapo mfululizo, Old Trafford wakibuni mbinu mpya za
kuhamasisha ushindi kwa kutenga Jukwaa maalum la Waimbaji na huko
Emirates Meneja Arsene Wenger amshangaa Mchezaji wake Aaaron Ramsey....
MOURINHO NA KICHAPO
Jose Mourinho amekubali kuwa kipigo cha
2-1 walichoshushiwa na FC Basel Jana Usiku kwenye Mechi ya UEFA
CHAMPIONS LIGI, UCL, ni jukumu lake analopaswa kuwajibika na pia kukiri
kuwa kichapo hicho ni hatua moja nyuma kwao.
Hicho ni kipigo cha pili mfululizo kwa
Chelsea baada ya Wikiendi pia kufungwa Bao 1-0 na Everton katika Mechi
ya Ligi Kuu England.
Na Mourinho amesema: “Mimi ndie Meneja.
Mimi ndie mwenye jukumu la kila kitu. Hasa baada ya matokeo mabaya.
Katika wakati mzuri nataka kila Mtu ang’are na wakati mbaya kila Mtu
atulie. Kesho nitaamka bila tabasamu usoni lakini Saa 1 Asubuhi nitaanza
kufanya kazi kwa bidii kusaka Pointi 3 kwa Fulham. Mechi ijayo
tunakwenda Bucharest na lazima tupate Pointi ili turudi kwenye UCL.
Hatutaki kucheza EUROPA LIGI!”
MAN UNITED NA NYIMBO
Manchester United watafanya majaribio
Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya UCL dhidi ya Real Sociedad kwa
kuweka eneo moja la Jukwaa kuwa sehemu maalum ya Washabiki ambao
watakuwa wakiimba Nyimbo za kuhamasisha.
Mpango huu ulitaka kujaribiwa Siku za
nyuma lakini ukapingwa na Polisi kwa vile eneo la Jukwaa lilopangwa
kuwaweka Waimbaji lilikuwa ni maalum kwa Washabiki wa Timu za Upinzani
na ilibidi Mashabiki hao wahamishwe na kuwekwa kwenye Jukwaa jingine
nyuma ya Maeneo ya Mabenchi ya Ufundi wa Timu kitu ambacho Polisi
walikiona ni hatari.
Lakini safari hii Klabu imeunga mkono
ombi la Mashabiki wao wa kuwa na Jukwaa la Waimbaji ili kuongeza sauti
katika kuhamasisha Timu yao kwenye Mechi.
Inatarajiwa eneo hilo maalum la Jukwaa
kwa ajili ya Waimbaji litakuwa na Washabiki 1,400 kwenye upande wa
Kusini Mashariki hapo Oktoba 23 wakati wa Mechi na Real Sociedad.
Nae Kiungo wa Man United, Michael
Carrick, ameunga mkono hatua hii kwa kutoa kwenye Akaunti yake ya
Twitter posti: “Ni wazo zuri sana kuwa na eneo la Waimbaji. Kama
ningekuwa naenda kama Shabiki hapo ndio ningetaka niwe….!!”
WENGER NA BUTAA KWA RAMSEY!
Bosi wa Arsenal Arsene Wenger amesema ufungaji Magoli wa Aaron Ramsey kwa sasa ni kitu kinachoshangaza.
Jana Usiku, Ramsey alifunga Bao moja
wakati Arsenal wanaichapa Marseille 2-1 katika Mechi ya UCL na hilo ni
Bao lake la 6 Msimu huu.
Wenger amekiri: “Hakika sikutegemea yeye
kufunga Bao nyingi namna hii lakini ameonyesha kuongezeka ubora wake
katika pasi zake na kiwango cha ufundi. Hilo ni muhimu kwani mara nyingi
huchomoza sehemu muhimu kwenye eneo la Penati.”
++++++++++++++++++++++
Ramsey apiga 6 Msimu huu:
18 Septemba: Bao moja dhidi ya Marseille, ushindi wa in 2-1
14 Septemba: Goli 2 walipoifunga Sunderland 3-1
27 Agosti: Goli 2 Mechi ya Marudiano na Fenerbahce kwenye UCL
21 Agosti: Goli 1 walipoifunga Fenerbahce Mechi ya Kwanza ya UCL
++++++++++++++++++++++
Wenger aliongeza "Kufunga Mabao kunatokea kwa mzunguko na kitu muhimu ni ubora wake kimchezo."
Mwaka 2010 Ramsey, mwenye Miaka 22,
alivunjwa Mguu sehemu mbili na Beki wa Stoke City Ryan Shawcross na
kukaa nje ya Uwanja kwa Miezi 9.
Jumamosi Arsenal watacheza Uwanjani kwao Emirates na Stoke City kwenye Mechi ya Ligi.
Comments
Post a Comment