MJADALA WA MUSWADA WA MABADILIKO YA SHERIA YA KATIBA WALAZIMIKA KUSIMAMA KWA MUDA LEO BAADA KUTOKEA HALI YA KULUMBANA KWA WABUNGE
Mara
baada ya kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa hapo kwa Waziri mkuu
na kufuatiwa na kipindi cha maswali na majibu bungeni kwa mujibu wa
ratiba ya bunge ilikuwa ni zamu ya wabunge kuendelea kuchangia muswaada
wa marekebisho ya sheria ya katiba wa mwaka 2013.
Hata
hivyo baadhi ya wabunge wakasimama na kuomba muongozo wa spika
wakiitaka serikali kuuondoa muswaada huo bungeni kwa ajili ya
kurekebisha mapungufu kadhaa mojawapo ikidaiwa kuwa baadhi ya taasisi
na hata upande wa Zanzibar haukushirikishwa kikamilifu katika utoaji wa
maoni yao huku Mh Ali Hamis Seifu mbunge wa Mkoani kupitia CUF akitoa
hoja ya kutaka mjadala wa katiba uahirishwe,ambapo uamuzi wake ni ama
spika akubali ama akatae au awahoji wabunge na ndipo naibu spika
alipoamua kuwahoji wabunge.
Hatua
hiyo haikuonekana kuwaridhisha wabunge wa kambi ya upinzania na kutaka
kura zihesabiwa suala lililoafikiwa na naibu spika Job Ndugai na kutaka
kura kuhesabiwa kwa mtindo wa ndio na siyo.
Baada
ya kumalizika kwa zoezi hilo naibu spika Job Ndugai akalichukulia kuwa
ni kielelezo cha demokrasia ya kweli na kuruhusu wabunge kuendelea
kuchangia na kumpa fursa Mh Augustine Lyatonga Mrema mbunge wa Vunjo na
ndipo akasimama kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kutaka kuzungumza
huku akizuiwa na naibu spika.
Kitendo
cha kuamuru askari kumtoa nje Mh Mbowe kikasababisha vurugu kubwa baina
ya wabunge wa vyama vya upinzani waliokuwa wakipinga Mh Mbowe kutolewa
nje dhidi ya askari wa bunge na jambo lililosababisha waziri mkuu Mh
Mizengo Pinda kushindwa kushuhudia na kuamua kutoka nje .
Wakati
wakitoka nje ya bunge,nje ya bunge Mh Joseph Mbilinyi akadai kupigwa
teke la uso na mmoja wa askari wa bunge na kutaka kumlipizia kisha
kuzuiwa na baadhi ya wabunge wenzie na kuondoka katika viwanja vya bunge
akiwa ndani ya gari la kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Mh
Freeman mbowe.
Kitendo
cha wabunge hao kutoka nje ya bunge hakikumzuia naibu spika Mh Job
Ndugai kuruhusu wabunge kuendelea na mjadala kama kawaida na kumpa fursa
Mh Augustine Lyatonga Mrema na kutangaza kuwasamehe wabunge hao wa
upinzani.
Comments
Post a Comment