MAUZO YA OZIL: VILABU VITATU VYA UJERUMANI KUNUFAIKA NA €50 MILLIONI WALIZOLIPA ARSENAL
Ozil alianza maisha yake ya soka katika klabu hiyo ya zamani ya Bundesliga kabla ya kuhamia Schalke -- iliyopo katika vitongoji vya nyumbani huko Gelsenkirchen -- mnamo mwaka 2005 akiwa na miaka 16. Mwaka mmoja baadae, August 12, 2006, alicheza mechi yake ya kwanza ya Bundesliga akiitumikia Schalke Royal Blues katika mechi ya sare ya 1-1 dhidi ya Eintracht Frankfurt.
Baada ya kucheza mechi 30 akiwa na Schalke, Ozil alihamia Werder Bremen mwaka 2008, kabla ya kuhamia Madrid kwa ada ya uhamisho wa €18 million kufuatiwa kuonyesha kiwango kizuri katika michuano ya kombe la dunia.
Vilabu vyote vitatu vya Ujerumani vitapata mgawo wa fedha za mauzo ya Ozil. Kwa mujibu wa kanuni ya FIFA, vilabu vyote alivyochezea Ozil kutoka alipokuwa na umri wa miaka 12 mpaka 23 vinapaswa kulipwa fidia ya kumfundisha soka kwa maana ya mazoezi, kwa maana hiyo kila klabu itapata mgawo kutoka kwenye 5% ya €50m .
Namna mgawanyo utakavyokuwa ni kwamba Schalke na Rot-Weiss Essen watapata shea ya 30% ya fidia kutoka kwenye fedha ya mgawo, huku asilimia 70 zilizobakia zikigawanywa kwa Werder Bremen na Real Madrid.
Comments
Post a Comment