KOCHA KIM PAULSEN WA TAIFA STAR AFUNGUKA NA MECHI YA GAMBIA SEPT 7 2013


 Licha ya kupoteza nafasi ya kufuzu kushiriki fainali za kombe la dunia, kocha mkuu wa timu ya soka ya Taifa,  Taifa Stars Kim Paulsen amesema lengo lake ni kuona kikosi chake kinamaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi C kwa kuifunga Gambia katika mchezo wa mwisho wa kukamilisha ratiba utakaochezwa Septemba 7 nchini humo.
Stars ambayo ilianza vema michuano hiyo na kuweka hai matumaini ya kufuzu kushiriki fainali za kombe la dunia zitakazochezwa mwakani nchini Brazil kabla ya kupoteza mechi mbili dhidi ya Morroco ugenini na dhidi ya Ivory Coast hapa nyumbani na kujikuta ikiangukia katika nafasi ya tatu kwenye kundi lake linaloongozwa na tembo wa Ivory ccast na kufuatiwa na Morrocco huku Gambia ikikamata mkia.
Akizungumza kwenye kambi ya timu hiyo jijini dar es salaam  Kim Paulsen amesema baada ya kupoteza nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano ya kufuzu kombe la dunia sasa amejikita katika kutengeneza kikosi imara kwa ajili ya mashindano ya kufuzu fainali za afrika . Hata hivyo katika mchezo huo dhidi ya Gambia Kim atalazimika kuwakosa nyota wake wanne kutokana na kuwa majeruhi ambao ni Kelvin Yondani, Athumani Idd Chuji, Shomari Kapombe na John Boko 'adebayo'
Stars imeingia kambini tangu septemba 29 kujiandaa na mchezo huo na imekuwa ikifanya mazoezi katika uwanja wa kumbukumbu ya Karume na uwanja wa taifa ambapo wachezaji wa kimataifa wa tanzania wanaokipiga katika klabi ya TP Mazembe ya DRC Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata wanatarajia kujiunga na wenzao kambini katikati ya wiki hii tayari kwa safari ya kwenda Gambia.

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

NINI MAANA YA MAPENZI

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU