CHELSEA YAPIGWA KWAO STAMFORD BRIDGE!!
>MESSI APIGA HETITRIKI, BARCA 4 AJAX 0!!
>DORTMUND YALALA!!
MAKUNDI E hadi H ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, Usiku huu wamecheza Mechi zao za kwanza kwa
Chelsea kubondwa kwao Stamford Bridge na Supastaa Lionel Messi kupiga
hetitriki na kuipa ushindi Barcelona huku Borussia Dortmund, Timu
iliyofika Fainali ya UCL Msimu uliopita, kuchapwa Ugenini.
PATA ZAIDI:
---------------------------
MATOKEO:
Jumatano 18 Sep 2013
FC Schalke 3 FC Steaua Bucureşti 0
Chelsea 1 FC Basel 2
Olympique de Marseille 1 Arsenal 2
SSC Napoli 2 Borussia Dortmund 1
FK Austria Wien 0 FC Porto 1
Club Atlético de Madrid 3 Football Club Zenit 1
AC Milan 2 Celtic FC 0
FC Barcelona 4 AFC Ajax 0
-----------------------------
KUNDI E
-FC SCHALKE 3 FC STEAUA BUCUREŞTI 0
Schalke wameichapa Steau Bucharest Bao 3-0 kwa Bao za Draxler, Boateng na Uchida.
-CHELSEA 1 FC BASEL 2
Jose Mourinho leo ameanza kwa mkosi UCL
baada ya kuchapwa Nyumbani Bao 2-1 na FC Basel ya Uswisi na hiki ni
kipigo cha pili mfululizo kwake kufuatia kufungwa Wikiendi iliyopita
kwenye Ligi na Everton.
Chelsea walitangulia kufunga kwa Bao la
Oscar mwishoni mwa Kipindi cha Kwanza lakini FC Basel walikuja juu na
kupiga Bao mbili katika Dakika za 71 na 82 Wafungaji wakiwa Mohamed
Salah, Kijana wa Egypt, na Marco Streller.
VIKOSI:
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Luiz, Cole, Oscar, van Ginkel , Lampard, Willian, Eto'o, Hazard
Akiba: Schwarzer, Mata, Mikel, De Bruyne, Ba, Terry, Azpilicueta.
Basel: Sommer, Voser, Schar, Ivanov, Safari, Salah, Diaz, Frei, Stocker, Sio, Streller
Akiba: Vailati, Philipp Degen, Ajeti, David Degen, Delgado, Sauro, Xhaka.
Refa: Daniele Orsato (Italy)
KUNDI F
-OLYMPIQUE DE MARSEILLE 1 ARSENAL 2
Bao za Theo Walcott na Aaron Ramsey
Usiku huu zimeendeleza ubabe wa Arsenal kwa Klabu za France walipoichapa
Marseille Bao 2-1 huko kwao France.
Bao la Marseille lilifungwa kwa Penati
katika Dakika za Majeruhi baada ya Ramsey kumchezea Faulo Andre Ayew na
Penati kupigwa na Ndugu yake Jordan Ayew na kufunga.
VIKOSI:
Marseille: Mandanda, Fanni, N'Koulou, Lucas Mendes, Morel, Romao, Imbula, Payet, Valbuena, Andre Ayew, Gignac
Akiba: Samba, Mendy, Cheyrou, Jordan Ayew, Lemina, Thauvin, Khelifa.
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Flamini, Ramsey, Walcott, Wilshere, Ozil, Giroud
Akiba: Fabianski, Vermaelen, Monreal, Jenkinson, Miyaichi, Akpom, Hayden.
Refa: Olegario Benquerenca (Portugal)
-SSC NAPOLI 2 BORUSSIA DORTMUND 1
Napoli wameipiga Borussia Dortmund Bao
2-1 katika Mechi ambayo Kocha wa Dortmund, Jurgen Klopp, alitolewa nje
ya Uwanja na pia Mchezaji wao Weidenfeller kupewa Kadi Nyekundu katika
Dakika ya 45.
Bao za Napoli zilifungwa na Gonzalo
Higuian katika Dakika ya 29 na Insigne, Dakika ya 67 na lile la Dortmund
kufungwa na Zuniga katika Dakika ya 87.
VIKOSI:
Napoli: Reina; Maggio, Albiol, Britos, Zuniga; Inler, Behrami; Callejon, Hamsik, Insigne; Higuain
Akiba: Rafael, Cannavaro, Armero, Dzemaili, Pandev, Mertens, Mesto
Borussia Dortmund: Weidenfeller; Schmelzer, Subotić, Hummels, Grosskreutz; Şahin, Bender; Reus, Mkhitaryan, Blaszczykowski; Lewandowski
Akiba: Langerak, Kirch, Aubameyang, Gunter, Hofmann, Schieber, DurmKUNDI G
-FK AUSTRIA WIEN 0 FC PORTO 1
Bao la Dakika ya 55 la Gonzalez limewapa FC Porto ya Ureno ushindi wa Ugenini wa Bao 1-0 dhidi ya Austria Wien.
-CLUB ATLÉTICO DE MADRID 3 FC ZENIT ST PETRSBURG 1
Atletico Madrid wameichapa Zenit St Petersburg Bao 3-1 huku Bao zao zikifungwa na Miranda, Turan na Leo.
Bao la Zenit limefungwa na Hulk.
KUNDI H
-AC MILAN 2 CELTIC 0
AC Milan walifunga Bao mbili ndani ya Dakika 3 za Kipindi cha Pili na kuibwaga Celtic Bao 2-0.
Bao la kwanza lilipatikana baada ya
Emilio Izaguirre wa Celtic kujifunga mwenyewe kufuatia shuti la Cristian
Zapata katika Dakika ya 82 na la pili kufungwa na Sulley Muntari baada
ya Kipa Fraser Forster kuitema frikiki ya Mario Balotelli katika Dakika
ya 85.
VIKOSI:
AC Milan: Abbiati, Zaccardo, Zapata, Mexes, Constant, Muntari, De Jong, Nocerino, Matri, Birsa, Balotelli
Akiba: Amelia, Robinho, Poli, Cristante, Emanuelson, Benedicic, Iotti.
Celtic: Forster, van Dijk, Lustig, Ambrose, Izaguirre, Brown, Matthews, Mulgrew, Commons, Samaras, Stokes
Akiba: Zaluska, Biton, Boerrigter, Balde, Rogic, Pukki, McGeouch.
Refa: Wolfgang Stark (Germany)
-FC BARCELONA 4 AFC AJAX 0
Huko Nou Camp, FC Barcelona wameikung’uta Ajax Bao 4-0 kwa Bao za Lionel Messi, Bao 3, na moja kufungwa na Gerard Pique.
Ajax walipata Penati mwishoni iliyopigwa na Kolbeinn Sigthorsson lakini Kipa Valdes akaicheza.
MECHI ZIFUATAZO:
Jumanne 1 Oktoba 2013
FC Basel 1893 v FC Schalke 04
FC Steaua Bucureşti v Chelsea FC
Borussia Dortmund v Olympique de Marseille
Arsenal FC v SSC Napoli
Football Club Zenit v FK Austria Wien
FC Porto Club v Atlético de Madrid
AFC Ajax v AC Milan
Celtic FC v FC Barcelona
Jumatano 2 Oktoba 2013
FC Shakhtar Donetsk v Manchester United FC
Bayer 04 Leverkusen v Real Sociedad de Fútbol
Juventus v Galatasaray A.Ş.
Real Madrid CF FC København
Paris Saint-Germain v SL Benfica
RSC Anderlecht v Olympiacos FC
Manchester City FC v FC Bayern München
PFC CSKA Moskva v FC Viktoria Plzeň
Comments
Post a Comment