WABUNGEWAMCHACHAMALIA WAZIRI Mh. WILLIAM LUKUVI KUTAJA WAHUSIKA WA DAWA ZA KULEVYA

.
 Kauli ya waziri wa nchi ofisi ya waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge Mh. William lukuvi ya "hakuna mbunge hata mmoja atakayesalia salama endapo serikali itayataja majina ya watu wanaotajwa kuhusika katika biashara ya dawa za kulevya" imechukua  sura mpya baada ya baadhi ya wabunge kumtaka kuyataja majina hayo bungeni au kuifuta kauli yake.
Kauli iliyowafanya baadhi ya wabunge kutopata usingizi na kumfanya mbunge Simanjiro Mh christopher Ole Sendeka kuomba muongozo wa spika chini ya kanuni ya 68 saba kwa madai kuwa kauli hiyo si tu inalidhalilisha bunge bali pia wabunge hao watakosa sehemu za kuficha nyuso zao kwa wale ambao hawafahamu hata namna dawa hizo zinavyofanana.
Baada ya kuuomba uongozo huo,naibu spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania mh job ndugai akatoa fursa kwa waziri husika kutoa maelezo ambapo licha ya kukiri kulijibu swali hilo ameongeza kuwa serikali hii inayoongozwa kwa misingi ya sharia kamwe haitakubali kutangaza orodha ya majina hayo ambayo amedai kuwa ni nyingi sana kabla ya kufanya uchunguzi na kujiridhisha na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria watuhumiwa.

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

NINI MAANA YA MAPENZI

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU