TUNDA MAN AAMBULIA AIBU KUTOKANA NA KESI YA MADAI YA LAKI NANE



486652_458703697506379_1407667217_n


Taarifa tulizozipata ni kuwa Tunda man alikopa pesa kwa Mwanadada mmoja ambae hakupenda jina lake liwekwe mtandaoni kiasi cha laki nane kwa maelewano atamlipa baada ya muda kupita.
Akizungumza na Kituo kimoja cha radio dada huyo anadai baada ya muda kupita ikabidi antafute Tunda Man ili amkumbushe madai anayomdai, lakini haikuwa kama yule dada alivyotegemea kwani aliambulia matusi, na wakati mwingine akijaribu kumpigia Tunda simu haipokelewi, ndipo dada huyo alipoamua kwenda polisi ili afungue kesi ya madai
Baadae Tunda alitafutwa ndipo akakubali kuwa atamlipa kwa awamu tatu na awamu ya kwanza ilikuwa tarehe 12/08/2013 lakini tunda hakutokea kulipa deni japo waliandika makubaliano
Baada ya kuona kimya japo waikubaliana ndipo maaskari polisi walipoamua kwenda nyumbani kwa Tunda man ili kumkamata lakini hawakufanikiwa kwani Tunda aliwaona na akaamua kukimbia

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

NINI MAANA YA MAPENZI

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU