PICHA ZA UZINDUZI WA "FOOLISH AGE" YA LULU MICHAEL
MSANII wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael 'Lulu', usiku wa kuamkia leo amefanikisha zoezi la uzinduzi wa filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Foolish Age .
Baada ya move hiyo kali ya dakika 120 iliyooesha ukali wa staa huyo kuoneshwa kwa dakika 20 tu na kubakisha zingine 100 kusubiri wateja kuziona majumbani kwao alipanda jukwaani kujitambulisha na kutoa shukrani kwa wamepenzi wa tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa muitikio wao alipanda na kuimba wimbo huo wa Yahaya.
Akianzia kuimba kiitikio cha wimbo huo akiwa Back Stage, Lulu aliwashangaza watu pale alipomudu vyema wimbo huo kiasi cha mashabiki ‘Mapedeshee’ wakiongozwa na Pedeshee Rich Rich, kupanda jukwaani na kumtunza fedha kibao ambazo hakika zilimpagawisha msanii huyo na mwisho wa wimbo huo alisema mziki unalipa.
Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, na kuhudhuriwa na mastaa kibao wa tasnia mbalimbali hapa Bongo, wakiwemo; Judith Wambura 'Lady Jaydee', ambaye alitumbuiza sambamba na Barnaba na Amini.
Comments
Post a Comment