KAULI YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA YA IBUA HOJA

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, ameunga mkono hatua zinazochukuliwa na Jeshi la Polisi katika baadhi ya maeneo nchini za kuwapiga wananchi. Pinda alitoa kauli hiyo bungeni jana, wakati akijibu swali bungeni akiwataka Polisi kuendelea kutembeza bakora bila woga kwa wananchi wanaokaidi amri zao.

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Mutaza Mangungu, ambaye aliitaka Serikali kuweka wazi kiini cha matatizo ya vurugu badala ya kuwalaumu wanasiasa.

Katika swali hilo, Mangungu alisema vyombo vya dola vimeingia katika lawama kwa kudaiwa kuwapiga wananchi bila sababu, huku akitolea mfano wa matukio ya Arusha na Mtwara.

Katika majibu yake, Pinda alisema Serikali imechoshwa na vitendo vya vurugu vinavyoendelea nchini, hivyo kwa yeyote atakayekaidi amri ya vyombo vya dola anastahili kupigwa.

Pinda alisema, vyombo vya dola havipaswi kulaumiwa na kusisitiza kuwa mtu akiambiwa asifanye hiki akaamua kukaidi, atapigwa tu kwa maana hakuna namna nyingine.

Katika kipindi hicho cha maswali ya papo kwa hapo, Pinda aliwapa kichwa polisi badala ya kujibu swali lililoulizwa na mbunge aliyetaka kujua Serikali imebaini kwa kiasi gani kiini cha vurugu badala ya kuwalaumu wanasiasa.

Kauli kama hiyo haikupaswa kutolewa na kiongozi mkubwa wa Serikali kama Pinda, kwani kwa kauli hiyo polisi watazidisha kuwapiga wananchi hata kama haistahili.

Tunafahamu yapo mazingira ambayo Jeshi la Polisi wanatakiwa kutumia nguvu wakati wanapotekeleza majukumu yao, lakini katika hili la kupiga tu kisa wao ni polisi hatuliungi mkono.

Kwa mujibu wa Katiba ya nchi, chombo cha mwisho chenye mamlaka ya kutoa adhabu ni mahakama, Jeshi la Polisi kazi yake ni kuhakikisha ulinzi wa raia na mali zake.

Inapofika mahala askari polisi anatembeza mkong’oto kwa wananchi ni wazi kuwa amekwishatoa hukumu na ndiyo maana anampa adhabu hiyo ya kipigo. Swali hapa ni kwamba, mamlaka ya kuhukumu polisi kayatoa wapi?

Katiba yetu inaruhusu wananchi kukusanyika na hata kuandamana kama haki zao za msingi, hapa ni wajibu wa Jeshi la Polisi kuwalinda ili watimize haki yao ya msingi na si kuwapiga.

Tunapatwa na mshangao mkubwa, pale waziri mkuu anasema mwananchi anayekaidi amri ya polisi apigwe. Hivi huyu raia hana haki ya kupingana na polisi hata kama anaona haki yake inapokwa?

Kauli ya Pinda imekaa kiutawala zaidi badala ya kiuongozi, kwani haiwezekani kwa nchi kama Tanzania inayoongozwa kwa mujibu wa sheria, polisi wakatumia mabavu zaidi kuliko busara.

Tunalisihi Jeshi la Polisi linalofuata misingi ya sheria, halina budi kuzingatia haki za raia pamoja na haki za binadamu zilizoainish

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU

NINI MAANA YA MAPENZI