Pamoja na hali mbaya uwanjani – Man United wavunja rekodi ya mapato

_72928204_rc3hx3vo
Manchester United imeripoti taarifa ya kuongezeka kwa mapato ya klabu hiyo kwa 11.6% kwa awamu ya pili ya mwaka wa kifedha wa klabu hiyo.
Mabingwa hao
wa Barclays Premier League wamesema mapato yao yameongezeka kutokana ukuaji wa biashara yao ya matangazo na kuuza haki za matangazo ya TV ya kuonyesha mechi zao.
Mapato ya kuanzia kipindi cha October–December yamekuwa mpaka kufikia kiasi cha £122.9m.
Matangazo ya kibiashara yaliongezeka kwa asilimia  18.8%, wakati biashara ya kuuza haki za matangazo ya TV kwa ajili ya mechi zao yalipanda kwa asilimia 18.7%.
Klabu hiyo ilifanikiwa kupata udhamini wa makumpuni sita ya kibiashara.
CEO wa klabu hiyo  Ed Woodward alisema kwenye taarifa rasmi:  ”Kwa mara nyingine tena tumeweka rekodi ya kuingiza mapato makubwa kutokana na mchango mkubwa tunaopata kutoka washirika wetu wa kibiashara, hali hii inakuja pamoja na kuwa hatufanyi vizuri sana uwanjani, ukiangali nafasi tunayoshika uwanjani, ni jambo la kusikitisha na kila mmoja wetu anajua hilo.”
United kwa sasa wanashika nafasi  7 kwenye ligi na wanaweza kukosa nafasi ya kushiriki kwenye Champions League kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1995

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU

UMUHIMU WA KUJIFUNZA SAIKOLOJIA