Posts

VIWANGO VIPYA VYA ALAMA ZA UFAULU KIDATO CHA NNE NA SITA VYATOLEWA:

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI UPANGAJI WA VIWANGO VYA ALAMA, MATUMIZI YA ALAMA ENDELEVU YA MWANAFUNZI NA UFAULU UTANGULIZI Wizara imekusanya maoni ya Wadau wa Elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama (Grade Ranges) katika Mitihani ya Kuhitimu Kidato cha Nne na cha Sita pamoja na Matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi (Continuous Assessment ama  CA ) kwa ajili ya kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi. Maoni ya wadau yamekusanywa kwa sababu kwa muda mrefu sasa upangaji wa viwango vya alama vinavyotumika na utaratibu wake katika mitihani ya kuhitimu Kidato cha Nne na Kidato cha Sita umekuwa haufanani pamoja na kwamba mitihani hiyo yote ni ya elimu ya sekondari. Pia mfumo masuala mbalimbali ya mitihani katika elimu ya sekondari umekuwa na miundo tofauti ikiwemo ule unaotumika shuleni na ule wa Baraza la Mitihani la Taifa. Kwa sasa kuna miundo mikuu miwili katika mfumo huo. Muundo wa Kwanza ni upangaji ...

JENEZA LA DIAMOND LAIBUA MAZITO

Image
Stori: Shakoor Jongo na Musa Mateja STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye hakaukiwi na stori, safari hii amekuja na mpya baada ya kuibuka na jeneza lenye msalaba ambalo limeibua maswali mazito, Risasi Mchanganyiko linakupasha

Tanzania: Tunaweza kujitoa A. Mashariki

Image
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete Serikali ya Tanzania imesema inatafakari ushiriki wake ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na inaweza kujitoa ndani ya Jumuiya hiyo iwapo itaendelea kutengwa katika baadhi ya vikao. Aidha imesema Tanzania haitambui vikao vinavyofanywa na nchi tatu zilizopo ndani ya Jumuiya hiyo ambazo zimekuwa zikizitenga Tanzania na Burundi

Arsenal nje ya kombe la Capital One

Image
Juan Mata wa Chelsea akisherekea bao dhidi ya Arsenal Katika mashindano ya Capital one huko uingereza Arsenal ambao wako kileleni mwa ligi kuu ya uingereza waligaragazwa bila huruma na Chelsea kwa mabao mawili kwa bila. Lakini Chlesea walipokuwa wakiwatesa the Arsenal nyumbani kwao Manchester United waliwachapa Norwich kwa mabao manne kwa bila. Hii inafanya Man u Kushinda mara sita mfulululizo, bila shaka na kumpa Moyes matumaini ya kufanya vizuri katika ligii ya Uingereza halikadhalika kombe hilo la Capital one

Yaya Toure azuru Kenya. Kunani?

Image
Yaya Toure Mchezaji maarufu wa timu ya Manchester City Yaya Toure, amewasili mjini Nairobi Kenya kwa uzinduzi wa muungano mpya wa kukabiliana na uwindaji haramu kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mazingira (UNEP). Muungano huo umeanzishwa ili kukabiliana na uwindaji haramu wa wanyama pori haswa Ndovu ambao wanakabiliwa na tisho la kudidimia kutokana na uwindaji haramu barani Afrika. Toure, mshindi wa tuzo la mchezaji soka bora zaidi Mwafrika kwa miaka miwili mfululizo, 2011 na 2012 ataeleza kwanini amekubali kushirikiana na muungano huo kupambana dhidi ya uwindaji haramu na nini hasa jukumu lake

MBEYA CITY FC YAIBAMIZA TANZANIA PRISONS KWA MAGOLI 2-0

Image
 Mashabiki wa Mbeya City Fc wakishangilia Goli la Kwanza   Mashabiki wa Mbeya City Fc wakishangilia Goli la Pili  Mpira Unaendela ....

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU

Image
Unaweza kuzidharau mbegu za maboga, lakini ni miongoni mwa mbegu zenye faida kubwa mwilini, zinazoweza kuzuia na kutibu hata magonjwa hatari yaliyoshindikana hospitalini. Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi uliokwishafanyika, zifuatazo ni faida za kifya mtu anazoweza kuzipata kwa kula mbegu za maboga, zikiwa mbichi ama zilizokaangwa: HUIMARISHA MOYO, MIFUPA Mbegu za Maboga (Pumkin Seeds), zina kiwango kingi cha madini aina ya Magnesium ambayo ni muhimu kwa afya ya moyo, uimarishaji mifupa, mishipa ya damu na ufanisi wa utumbo mpana. Magnesium imeonesha uwezo mkubwa wa kuzuia mshituko wa moyo na kiharusi