Posts

MULUGO AMEAHIDI KITITA CHA SH. MILIONI MBILI IWAPO TIMU YA MBEYA CITY ITAISHINDA TIMU YA YANGA LEO JIJINI MBEYA

Image
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songwe mkoani Mbeya ameahidi kitita cha sh. milioni mbili iwapo timu ya Mbeya City itaishinda timu ya Yanga ya Jijini Dar es salaam. Waziri Mulugo akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya amesema atahakikisha kuwa....

YANGA WASHAMBULIWA NA MASHABIKI WA MBEYA CITY WAKIINGIA KWENYE UWANJAWA SOKOINE - BASI LAVUNJWA VIOO

Image
Dakika chache zilizopita wakati basi la klabu ya Yanga likiwa linaingia katika uwanja wa sokoine mjini Mbeya limeshambuliwa na mashabiki wanaodhaniwa kuwa wa Mbeya City kwa kupigwa mawe, kitu kilichopelekea vioo vya gari hilo kupasuka. Mpaka sasa hakuna taarifa kama kuna mchezaji yoyote wa klabu hiyo aliyejeruhiwa.

MWAKYEMBE ATOA SIKU 2 KUWABAINI WAHUSIKA WA KUTOBOA BOMBA LA MAFUTA BANDARINI.

Image
Waziri wa uchukuzi Dkt. Harrisoni Mwakyembe amebaini wizi wa mafuta katika boya la mafuta mjimwema na kuagiza maskari wa usimamizi wa bandari Tanzania kuwakilisha majina ya wahusika ndani ya siku mbili. Mwakyembe ameyasema hayo wakati akizungumza n a wafanyakazi wa mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania (TPA) na kulaani kitendo cha baadhi ya watu kutoboa bomba hilo na kuunganishia mabomba yao madogo na kuyafungia kwenye maputo yenye uwezo wa kubeba mafuta kati ya lita....
Image
YANGA WAPEWA SIKU 14 KUWALIPA NSAJIGWA NA MWASIKA DENI LAO LA MILLIONI 15.5 Yanga imepewa siku 14 kuanzia leo (Septemba 13 mwaka huu) kuwalipa waliokuwa wachezaji wake msimu uliopita, nahodha Shadrack Nsajigwa na Stephen Mwasika wanaoidai klabu hiyo jumla ya..............

VATICAN SASA KUJADILI KUHUSU UWEZEKANO WA MAPADRI WAKATOLIKI KUOA..!!

Image
Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican, Askofu Mkuu Pietro Parolin . Suala la mapadri wa Kanisa Katoliki kuoa au la, limeibuka upya na tayari limeanza kuzua mijadala mikali duniani. Mjadala wa sasa umeibuliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican, Askofu Mkuu Pietro Parolin ambaye aliteuliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo aliposema useja, yaani maisha ya utumishi ndani ya kanisa bila ndoa siyo imani, bali utamaduni na mazoea. Akizungumzia kauli hiyo, Msemaji wa Vatican, Federico Lombardi alisema kauli ya Askofu Parolin haipingani na mafundisho ya kanisa. Askofu Mkuu Parolin ambaye aliteuliwa karibuni na Papa Francis kushika wadhifa huo kutoka kwa Kardinali Tarcisio Bertone amenukuliwa na Gazeti la El Universal la Venezuela, Amerika ya Kati akieleza kuwa suala hilo linaweza kujadiliwa.

BAADA YA KUTWAA UBINGWA WA DUNIA SERIKALI KUMJENGEA NYUMBA YA KISASA FRANCIS CHEKA

Image
Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia mkuu wa mkoa wa Morogoro leo hii imemfanyia hafla fupi ya kumpongeza Bondia Francis Cheka aliyeiletea sifa kubwa nchi baada ya kushinda ubingwa wa dunia kwa kumtandika aliyekuwa bingwa wa dunia Phil Williams kutoka nchini Marekani.

ALIYEKUWA MISS TANZANIA 2006 AFUNGUKA SIFA 4 WANAUME WANAO MMEZEA MATE:

Image
 MREMBO anayefanya vizuri katika mambo mengi nchini, Jokate Urban Mwegelo (pichani) ametaja sababu nne zinazowafanya wanaume kumzimikia, akiwemo nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.  Akiandika katika mtandao wake wa Kidoti Life Style, Jokate, mshindi wa pili wa Miss Tanzania 2006, alizitaja sababu hizo kuwa ni kujiamini, kujitegemea, kupendeza na tabasamu muda wote.