YANGA WAPEWA SIKU 14 KUWALIPA NSAJIGWA NA MWASIKA DENI LAO LA MILLIONI 15.5
Yanga
imepewa siku 14 kuanzia leo (Septemba 13 mwaka huu) kuwalipa waliokuwa
wachezaji wake msimu uliopita, nahodha Shadrack Nsajigwa na Stephen
Mwasika wanaoidai klabu hiyo jumla ya.............. sh. milioni 15.5.
Uamuzi
huo umefanywa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Septemba 12 mwaka
huu) ambapo pamoja na mambo mengine ilisikiliza madai ya wachezaji hao.
Fedha
hizo ni ada ya usajili ambayo klabu hiyo ilikubaliana na wachezaji hao
wakati ikiwasainisha mikataba. Yanga imeshawalipa sehemu ya fedha
walizokubaliana na kiasi hicho ndicho bado hakijalipwa. Nsajigwa anadai
sh. milioni 9 wakati Mwasika ni sh. milioni 6.5.
Comments
Post a Comment