Posts

NAMBA ZA SIMU ZA MAWAZIRI ILI KUWATUMIA MAONI KUHUSU KODI YA SIMU

Kufuatia kauli za Serikali magazetini kuhusu mimi na kodi ya umiliki wa kadi za simu; nijibu tu kwa ujumla kwamba SITAACHA. Badala yake naomba kuwapatia namba zao: Makamba 0767783996 na Mgimwa 0754/0684765644, tunachohitaji ni kauli ya Serikali kuwa kodi imesitishwa na itaondolewa na sio siasa chafu. Kwa mliotaka msimamo wangu juu ya kauli ilinukuliwa jana tarehe 18 Julai 2013 na Gazeti la Majira kwamba Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba kwamba;  “Mnyika anaangalia upepo unakoelekea, akiona watu wanalalamika ndipo anaongea namsihi aache kufanya siasa katika jambo hili” , naomba kutumia mtandao huu kutoa majibu ya ujumla kwa maswali na masuala yote kama ifuatavyo: Nieleze kwamba sitaacha kufanya siasa kwenye jambo hili mpaka kodi hiyo itakapofutwa kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kubaki na fedha walau kidogo kwa maendeleo. Sitaacha kufanya siasa kwa sababu ndio kazi yangu ambayo wananchi walinichagua kuifanya ya kuwawaki...

tazama video ya Ben Pol - JIKUBALI 2013

Image

DUDE KUIGIZA KAMA YAHAYA KATIKA VIDEO MPYA YA LADY JAYDEE

Image
Msanii wa bongo movie anajulikana kwa jina la DUDE yeye ndie atakayecheza pati ya YAHAYA katika video mpya ya mwanadada LADY JAYDEE. Video hii imeanza kushutiwa leo(jana) jioni, kaa tayari kwa kumuona Dude akiwa kama Yahaya .najinsi alivyo weza kucheza kipengele icho ameweza kuonyesha kipaji chake kwa kumpa lady jaydee kampani katika kuuaanda video ya yahaya ambayo audio yake ina wika ivi mtaani na vyombo mbalimbali...  

BAADA YA MAN UNITED KUPELEKA OFA BARCA - FABREGAS ASEMA ANATAKA KUENDELEA KUBAKI CAMP NOU

Image
Siku chache baada ya kumkosa Thiago Alcantara inaonekana sasa Manchester United ipo njiani kumkosa mchezaji mwingine kutoka FC Barcelona , Cesc Fabregas. Hii inakuja baada ya kocha wa klabu hiyo  Tito Vilanova kusema kwamba ameongea na kiungo huyo wa Sp ain na ameambia na mchezaji huyo kwamba anahitaji kuendelea kubaki Camp Nou. Jana jumatatu iliripotiwa kwamba United walituma ofa ya kwanza ya kiasi cha £25.9 million  kwa ajili ya kumsajili Fabregas, ambaye amefeli kupata nafasi katika kikosi cha kwanza tangu aliporudi akitokea Arsenal . Lakini akiongea na waan dishi wa habari leo mchana, Vilanova amesema wazi kwamba Fabregas bado anataka kubaki kwenye klabu yake hiyo ya utotoni, na hana mawazo ya kuondoka kwa sasa .  "Nina fahamu kwamba tumepokea ofa kadhaa kutoka kwa vilabu tofauti. Niliongea na Cesc na ameniambia kwamba anataka kubaki. "Cesc hana mawazo ya kuondoka kwenda klabu nyingine. Anajua ushindani ni mku bwa hapa na ana ndoto za kuendelea kuwa ha...

ujio mpya wa Afande Sele akipewa sakoti na Belle 9 Dini Tumeletewa

Image

JESHI LA POLISI LATEUA ASKARI WA KUMFUATA AGNESS MASOGANGE ALIYENASWA NA MADAWA YA KULEVYA AFRIKA KUSINI

Image
Jeshi la Polisi litapeleka askari wake Afrika Kusini kuwahoji washiriki wa video za wasanii wa muziki wa Bongo fleva, Agnes Gerald ‘Masogange’ na mwenzake Melisa Edward waliokamatwa nchini humo na dawa za kulevya. Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa aliiambia  Mwananchi  kwa simu jana kuwa watawapeleka polisi kuwahoji na wanaamini wahusika watawaeleza wahusika wa mzigo huo. Wasichana hao walikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania wakiwa na kilo 150 za dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine. “Tutawapeleka askari wetu kuwahoji, tumekwishaanza uchunguzi wa hili...wote watakaohusika katika hili tutawakamata, lakini tunakwenda polepole hatua kwa hatua kuhakikisha tunawanasa wahusika sahihi,” alisema Nzowa. Naye Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege...