Posts
DUDE KUIGIZA KAMA YAHAYA KATIKA VIDEO MPYA YA LADY JAYDEE
- Get link
- X
- Other Apps
Msanii wa bongo movie anajulikana kwa jina la DUDE yeye ndie atakayecheza pati ya YAHAYA katika video mpya ya mwanadada LADY JAYDEE. Video hii imeanza kushutiwa leo(jana) jioni, kaa tayari kwa kumuona Dude akiwa kama Yahaya .najinsi alivyo weza kucheza kipengele icho ameweza kuonyesha kipaji chake kwa kumpa lady jaydee kampani katika kuuaanda video ya yahaya ambayo audio yake ina wika ivi mtaani na vyombo mbalimbali...
BAADA YA MAN UNITED KUPELEKA OFA BARCA - FABREGAS ASEMA ANATAKA KUENDELEA KUBAKI CAMP NOU
- Get link
- X
- Other Apps
Siku chache baada ya kumkosa Thiago Alcantara inaonekana sasa Manchester United ipo njiani kumkosa mchezaji mwingine kutoka FC Barcelona , Cesc Fabregas. Hii inakuja baada ya kocha wa klabu hiyo Tito Vilanova kusema kwamba ameongea na kiungo huyo wa Sp ain na ameambia na mchezaji huyo kwamba anahitaji kuendelea kubaki Camp Nou. Jana jumatatu iliripotiwa kwamba United walituma ofa ya kwanza ya kiasi cha £25.9 million kwa ajili ya kumsajili Fabregas, ambaye amefeli kupata nafasi katika kikosi cha kwanza tangu aliporudi akitokea Arsenal . Lakini akiongea na waan dishi wa habari leo mchana, Vilanova amesema wazi kwamba Fabregas bado anataka kubaki kwenye klabu yake hiyo ya utotoni, na hana mawazo ya kuondoka kwa sasa . "Nina fahamu kwamba tumepokea ofa kadhaa kutoka kwa vilabu tofauti. Niliongea na Cesc na ameniambia kwamba anataka kubaki. "Cesc hana mawazo ya kuondoka kwenda klabu nyingine. Anajua ushindani ni mku bwa hapa na ana ndoto za kuendelea kuwa ha...
ujio mpya wa Afande Sele akipewa sakoti na Belle 9 Dini Tumeletewa
- Get link
- X
- Other Apps
JESHI LA POLISI LATEUA ASKARI WA KUMFUATA AGNESS MASOGANGE ALIYENASWA NA MADAWA YA KULEVYA AFRIKA KUSINI
- Get link
- X
- Other Apps
Jeshi la Polisi litapeleka askari wake Afrika Kusini kuwahoji washiriki wa video za wasanii wa muziki wa Bongo fleva, Agnes Gerald ‘Masogange’ na mwenzake Melisa Edward waliokamatwa nchini humo na dawa za kulevya. Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa aliiambia Mwananchi kwa simu jana kuwa watawapeleka polisi kuwahoji na wanaamini wahusika watawaeleza wahusika wa mzigo huo. Wasichana hao walikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania wakiwa na kilo 150 za dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine. “Tutawapeleka askari wetu kuwahoji, tumekwishaanza uchunguzi wa hili...wote watakaohusika katika hili tutawakamata, lakini tunakwenda polepole hatua kwa hatua kuhakikisha tunawanasa wahusika sahihi,” alisema Nzowa. Naye Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege...
Nelson mandela angalia hali mahututi
- Get link
- X
- Other Apps
Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela angali hali mahututi ingawa madaktari wanaidhibiti hali yake. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya rais wa nchi hiyo Jacob Zuma. Mandela aliyekuwa rais wa kwanza mwafrika wa Afrika Kusini ana umri wa miaka 94, alilazwa hospitalini tarehe 8 mwezi Juni akiwa anaugua maradhi ya mapafu. Taarifa ya Zuma iliwashukuru wote waliomtumia ujumbe wa ugua pole Mandela nchini Afrika Kusini na kutoka kote duniani. Wiki jana Rais Zuma alikanusha madai kuwa Mandela hana fahamu tena.. Watu waliomuona wanasema kuwa anaweza kusikia na hata kuhisi. "tunashukuru umma wote kwa wale waliomuombea ili apate nafuu nje ya hospitali,'' ilinukuu taarifa ya Zuma ambayo ni ya kwanza katika siku tano zilizopita kuhusu hali ya Mandela. Bwana Mandela anasifiwa kote duniani kwa ushujaa wake alipokuwa anapigania uhuru wa ...