UFUGAJI WA NGURUWE
Utunzaji wa nguruwe mara nyingi hutegemea aina ya nguruwe,
njia na aina ya ufugaji. Kwa mfano nguruwe jike anayefugwa kwa ajili ya kuzaa
anahitaji kutunzwa tofauti na wale wanaonenepeshwa kwa ajili ya nyama.
Kadhalika nguruwe wanaweza kufugwa ndani ya banda au nje, kutegemea na ukubwa
wa shamba, fedha zilizopo kwa shughuli za ufugaji na aina ya nguruwe.
Utunzaji wa Nguruwe
Dume
Achaguliwe dume mwenye sifa bora ikiwa ni pamoja na
kutokuwa na kilema au ugonjwa wowote. Dume aliyechaguliwa, atenganishwe na majike
ili kuepusha kupanda wakati usiotakiwa. Inabidi nguruwe huyu asinenepeshwe, kwa
hiyo alishwe chakula bora kiasi cha kilo mbili hadi tatu kwa siku. Vile vile
apewe maji kila siku.
Kama anapanda chini ya mara tatu kwa wiki, alishwe
kilo mbili na nusu na kama anapanda zaidi ya mara tatu, alishwe kilo tatu kwa
siku. Ikiwa dume ni dhaifu, aongezewe nusu kilo ya chakula na kama amenenepa
sana apunguziwe nusu kilo ya chakula kwa siku. Ni muhimu awe na eneo la mita
mraba 9.3 ilikuwezakupata mazoezi ya mwili. Ikiwa sehemu ya kupanda
imetenganishwa eneo livve la mita mraba saba.
Nguruwe dume anaweza kutumika kwa kupandajike akiwa
na umri wa miezi minane hadi tisa. Kwa umri huu anaruhusiwa kupanda
jikemojakwajuma. Afikiapo miezi 10 anaruhusiwa kupanda majike mawili hadi
matatu kwajuma. Akiwana umri wa mwaka mmoja au zaidi ana uwezo wa kupandajike
mmoja kila siku kwa majuma mawili hadi malatu, kisha apumzike kwa muda wa
majuma mawili. Dume wakubwa wasitumike kupandajike wadogo kwani vvanaweza
kuleta madhara kama vile kuwavunja mgongo.
Ni vizuri nguruwe dume mmoja apandejike 15 hadi 20
kwa mwaka. Dume akizeeka au kuwa na ubovu wa miguu, achinjwe mara moja. Ni
muhimu dume aogeshwe kwa sabuni na dawa zinazoweza kuua wadudu na vijidudu
vinavyoweza kusababisha magonjwa. Banda na vifaa vinavyotumika visafishwe kila
siku.
Utunzaji Wa Nguruwe
Jike
Ili mfugaji aweze kupata mazao mengi na bora hana
budi kuchagua ngumwejike mwenye sifa zinazotakiwa. Nguruwe huyu ni vizuri awe
amezaliwa na mama anayezaa watoto wengi, mwenye kutoa maziwa mengi na mtunzaji
mzuri wa watoto. Tabia hizi zinarithiwa hata navizazi vingine vijavyo. Vile
vile awe na afyanzuri na chuchu nyingi zisizopungua 12.
Nguruwe jike anaweza kuzaa akiwa na umri wa miezi
mitano hadi sita. Ili kumzuia asibebe mimba mapema, ni vizuri atenganishwe na
dume afikiapo umri huo.
Afikiapo miezi nane hadi tisa au akiwa na uzito wa
kilo 130 ahaweza kupandishwa. Kabla ya kupandishwa nguruwejike apewe kilo 2.5
hadi tatu za chakula kwa siku. Nguruwe asipelekwe kwa dume mpaka atakapoonyesha
dalili zajoto.
· Dalili za Joto:
- Kutopenda kula chakula.
- Kupiga kelele ovyo.
- Kuhangaika kila mara.
- Hupenda kupanda au kupandwa na nguruwe wenzake.
- Sehemu ya uke huvimba na huwa nyekundu.
- Hukojoa mara kwa mara na hutoa ute mweupe usiokatika.
- Hutulia anapokandamizwa mgongoni.
- Kupiga kelele ovyo.
- Kuhangaika kila mara.
- Hupenda kupanda au kupandwa na nguruwe wenzake.
- Sehemu ya uke huvimba na huwa nyekundu.
- Hukojoa mara kwa mara na hutoa ute mweupe usiokatika.
- Hutulia anapokandamizwa mgongoni.
Dalili hizi sio lazima zionekane zote kwa wakati
mmoja hivyo ni jambo la muhimu kuwa mwangalifu.
Ili dalili hizi ziweze kuonekana vizuri, chumba cha
majike yanayotarajiwa kupandwa kinatakiwa kiwe karibu na cha dume. Joto hudumu
kwa muda wa siku mbili hadi tatu. Ngumwe Jike apandishwe mara anapokua kwenye
joto na kumdia tena katika muda wa masaa 12. Baada ya kupandishwa huchukua
miezi mitatu, wiki tatu, siku tatu (siku 114 hadi 119) hadi kuzaa. Ngumwejike
wawekwe kwenye banda lenye nafasi, hewa ya kutosha na uzio wa kutosha kwa ajili
ya mazoezi.
· Kutunza Nguruwe
Mwenye Mimba.
Nguruwe wenye mimba wanahitaji mazoezi zaidi ili
kuimarisha miguu na misuli yao, hivyo banda liwe na uzio wanapoweza kutoka na
kucheza. Sehemu ya uzio isiwe na unyevu ili wasipate magonjwa, ikiwezekana kuwe
na kivuli cha kuwakingajua.
Mandalizi ya Chumba cha Kuzalia
Wiki mbili hadi tatu kabla ya nguruwe kuzaa andaa
chumba cha kuzalia. Chumba hiki kiwekwe boriti au reli kuzunguka ili kutenga
sehemu ambayo itahifadhi watoto wasilaliwe au kukanyagwa na mama yao (angalia
mchoro sura ya tano).
Vile vile chumba hiki kiwe na sehemu ya kuweka
chombo cha kuongezeajoto, chakula na maji kwa ajili ya watoto.
Maandalizi Kabla ya Kuzaa
Wiki moja kabla ya kuzaa ngumwe aogeshwe vizuri kwa
maji safi na sabuni. Baada ya kuogeshwa anyunyiziwe dawa ili kuzuia wadudu wa
ngozi na apewe dawa ya minyoo. Kisha ahamishiwe kwenye chumba cha kuzalia.
Nguruwe mwenye mimba anahitaji kupewa chakula
kinacholeta nguvu na kujenga mwili. Katika mwezi wa kwanza apewe kilo 2 hadi
2.5 kwa nguruwe mwenye afya nzuri, akiwa dhaifu apewe kilo 3 kwa majuma matatu.
Mwezi wa pili mpaka siku ya tatu kabla ya kuzaa
alishwe kilo 3.5 za chakula. Siku ya tatu kabla ya kuzaa, chakula kipunguzwe
hadi kufikia kilo 2 kwa siku. Siku ya kuzaa asipewe chakula bali apewe maji tu.
Dalili za Kuzaa
Kuna dalili ambazo ngumwe huonyesha kabla hajazaa.
Dalili hizi zionekanapo kuna umuhimu wa kuwepo mwangalizl ili aweze kutoa
msaada kama itabidi, hasa kwa nguruwe anayezaa kwa mara ya kwanza.
· Kiwele na chuchu huwa kubwa kwa kujaa maziwa.
· Njia ya uke huvimba na kuwa nyekundu na mara nyingine hutoa maji mazito.
· Nguruwe huhangaika na hupumua kwa nguvu,
· Maziwa yanaweza kutoka yenyewe kwenye chuchu
· Hukojoa mara kwa mara
· Hukusanya majani na kuandaa mahali pa kuzalia
· Tumbo linapwelea na baadhi hupbteza hamu ya kula.
· Njia ya uke huvimba na kuwa nyekundu na mara nyingine hutoa maji mazito.
· Nguruwe huhangaika na hupumua kwa nguvu,
· Maziwa yanaweza kutoka yenyewe kwenye chuchu
· Hukojoa mara kwa mara
· Hukusanya majani na kuandaa mahali pa kuzalia
· Tumbo linapwelea na baadhi hupbteza hamu ya kula.
Utunzaji Baada ya Kuzaa
Mwangalizi ahakikishe kuwa watoto wananyonya na
kuwaweka mahali penyejoto la kutosha. Vitovu vikatwe na kuachwa sentimita tano
kwa kutumia vifaa visafi, na kisha paka dawa yajoto (lodine tincture) kuzuia
magonjwa.
Kondo la nyuma likidondoka litupwe na hakikisha
limetoka lote kwa kuhesabu vipande kulingana na idadi yawatoto. Endapo idadi
haikulingana, unashauriwa kumwona mtaalam wa mifugo aliyekaribu nawe.
Baada ya nguruwe kuzaa apewe ongezeko la kilo moja
ya chakula kila siku hadi siku ya nne. Kuanzia siku ya tano hadi ya nane apewe
hadi kilo nne. Baada ya hapo apewe kilo tatu na moja ya tatu ya kilo kwa kila
mtoto. Kwa mfano nguruwe mwenye watoto 12 apewe chakula kiasi cha kilo saba;
(kilo 3 + 1/3 x 12 = 7).
Vile vile apewe maji ya kutosha wakati wote.
Kumbuka nguruwe akilishwa chakula kingi, atanenepa sana na hatapata mimba kwa
urahisi na akibahatika kupata huweza kuharibika. Akilishwa chakula kidogo
hudhoofika, huzaa watoto dhaifu na hutoa maziwa kidogo. Siku ya kuwatenganisha
watoto na mama yao punguza chakula mpaka kilo mbili kwa siku. Siku inayofuata
ongeza hadi kufikia kilo 2.5 mpaka tatu kutegemea na afya ya mama.
Nguruwehurudi kwenyejoto baada ya siku tano hadi
kumi baada ya kuachisha kunyonyesha.
Utunzaji wa Watoto
· Ulishaji wa Maziwa ya Kwanza
Mara tu baada ya kuzaliwa hakikisha kuwa vitoto
vinanyonya maziwa ya kwanza. Maziwa haya ni muhimu kwani yana viinilishe vya
kujenga mwili, kuleta nguvu na kuongeza kinga dhidi ya maradhi.
Kama mama amekufa mara tu baada ya kuzaa na hakuna
nguruwe mwingine anayeweza kuwanyonyesha, wapewe maziwa ya kwanza ya ng’ombe.
Endapo yatakosekana wapewe mchanganyiko maalum wa maziwa ya ng’ombe.
· Joto
Watoto wa nguruwe huzaliwa bila manyoya na huwa
hawana mafuta mengi ya kutosha kuwapatiajoto mwilini. Kwenye sehemu za baridi
ni jambo la muhimu kuwapatiajoto kwa kutumia umeme au chemli.
· Kuzuia Upungufu wa Damu
Nguruwe huzaliwa wakiwa na upungufu wa madini ya
chuma. Halikadhalika maziwa ya mama yao huwa na upungufu wa madini hayo, hivyo
wasipopatiwa madini hayo hupata upungufu wa damu, hudhoofika na hatimaye hufa.
Ili kuepuka tatizo hili watoto wapatiwe madini ya
chuma kwa kutumia mojawapo ya njia zifuatazo:
- Kudunga sindano ya madini hayo kwenye misuli siku mbili hadi tatu
baada ya kuzaliwa.
- Kupaka madini ya chuma kwenye chuchu za mama.
Changanya kilo moja ya madini ya chuma kwenye lita
mbili za majimoto.
- Kuwanywesha maji yenye madini ya chuma mililita
moja na nusu kwa mwezi mmoja.
- Kuwapa udongo msafi.
- Watoto wanaotunzwa kwenye sakafu ya saruji au
mbao waruhusiwe kutoka nje ili kuweza kupata madini hayo kutoka kwenye udongo.
- Kuwapa vidonge vya madini ya chuma.
· UtoajiwaMeno
Siku chache baada ya kuzaliwa; meno kama sindano
huchomoza katika taya zote mbili; Meno haya humumiza na kusababisha vidonda
kwenye chuchu za mama wakati wanaponyonya. Hali hii humfanya mama kuwanyima
watoto maziwa na kuwapiga, hivyo husababisha vifo vya watoto. Vile vile wao kwa
wao huumizana.
Meno haya yafaa yakatwe kwa mkasi mkali na msafi.
Kama yasipokatwa huweza kumuumiza hata mhudumiaji.
· Kukata Mkia
Mkia wa nguruwe unaweza kukatwa mara tu baada ya
kuzaliwa ili wenyewe kwa wenyewe wasichezeane na kutafunana. Dawa ya lodine 5%
ipakwe penye kidonda mara tu baadaya kukata mkia.
· Kulisha Chakula cha Kwanza.
Watoto wapewe chakula maalum kidogo kidogo kuanzia
siku ya kumi baada ya kuzaliwa. Chakula hiki kinatakiwa kiwe na viinilishe vya
kujenga mwili, kuleta nguvu na kuzuia maradhi. Wakiwa na umri wa wiki tatu
wapewe gramu 450; wiki ya nne na ya tano wapewe gramu 680 kwa nguruwe kwa siku.
Endelea kuwapa chakula hiki mpaka siku ya kuachishwa kunyonya, na vile vile
wapewe maji kwa wingi.
· Kuhasi
Watoto madume ambao hawahitajiki kwa ajili ya
kuzalisha wahasiwe wakiwa na umri kati ya wiki tatu hadi sita.
Nguruwe waliohasiwa huwa wapole, hunenepa haraka,
huwa na nguvu na wazito kwa hiyo wanafaa kwa nyama na mafuta. Muone mtaalam wa
mifugo kwa ajili ya kuhasi nguruwe wako
· Vitambulisho
Ngumwe hupewa vitambulisho kabla ya kuwatenganisha
na mama yao kwa kuwaweka nambari kwenye masikio. Unashauriwa kumuona mtaalam wa
mifugo akupe ushauri wajinsi ya kuweka vitambulisho hivyo.
· Kutenganisha Watoto na Mama Yao.
Watoto wakifikia wiki nane watenganishe na mama
yao. Mama ahamishwe kwenye chumba na kuwaacha watoto ili kupunguza mgutusho wa
kuhamia mahali pengine. Unapowatenganisha hakikisha unawapa dawa ya minyoo,
unawakinga dhidi ya magonjwa na kuwatibu mara wanapougua.
Kukuza Nguruwe
· Walioachishwa Kunyonya
Nguruwe walioachishwa kunyonya wapewe chakula cha
kukuzia. Badilisha chakula kwa utaratibu maalum kwani kubadilisha chakula
ghafla kutoka cha watoto kuingia cha kukuzia kunaweza kusababisha matatizo ya
tumbo. Changanya chakula cha watoto na cha kukuzia katika uwiano ufuatao: -
Wiki
|
Chakula cha Watoto
|
Chakula cha Kukuzia
|
1
|
Sehemu 3
|
Sehemu 1
|
2
|
Sehemu 2
|
Sehemu 2
|
3
|
Sehemu 1
|
Sehemu 3
|
4
|
Sehemu 0
|
Sehemu 4
|
Inashauriwa kuwapa chakula kama ifuatavyo:-
Wiki
|
Kiasi kwa Siku (kilo)
|
8 - 12
|
1.0
|
12 - 18
|
1.5
|
18 - 23
|
2.0
|
23 - 30
|
3.0
|
Lisha marambili kwa siku. Piawapewe maji safi
yakutoshawakati wote.
Usafi wa chumba, vifaa na mazingira ni muhimu kila
siku. Pawe na vitu vya kuchezea kama vile minyororo au matairi ili kumpa
mazoezi, kuondoa upweke na kupunguza kupigana.
Endapo mkulima atahitaji nguruwe kwa ajili ya
kuzalisha, wakati mzuri wa kuchagua ni wanapofikia umri wa miezi mitatu na
kuendelea.
Nguruwe wanaweza kuchinjwa kwa ajili ya nyama
wakiwa wamefikia uzito wa kilo 60 hadi 90. Ikiwa watakuwa wametunzwa vizuri watafikia
uzito huo wakiwa na umri wa miezi 6 hadi 8
Comments
Post a Comment