KUTOKA UWANJANI SIMBA 1 YANGA 0
GOOOOOOOOO Dk 52, Okwi anaifungia Simba bao baada ya kumchungulia Barthez aliyekuwa mbele ya lango na kupiga mpira mrefu unaojaa moja kwa moja nyavuni.
KADI Dk 49 Nadir Haroub 'Cannavaro' analambwa kadi ya njano kwa kumkata Ibrahim Ajib
DK 47 Yanga wanaingia vizuri katika eneo la hatari la Simba, Tambwe anashindwa kuuwahi mpira, Murishid anaondosha
MAPUMZIKO:
DK 45 Tambwe anaweka kifuani vizuri anamuachia Msuva lakini anapaisha juu
DK 43 anapiga faulo Okwi inatoka kidogo nje ya lango la Yanga
KADI Dk 42, Niyonzima anamuangusha Singano na kupewa kadi ya njano
Dk 41, Tambwe anaingia katika eneo la hatari la Simba na kupiga shuti lakini linatua kwa ulaini katika mikono ya Ivo Mapunda.
Dk 36, Ivo anaokoa mpira miguuni mwa Ngassa anabaki Msuva peke yake na mpira anashindwa kulenga lango.
KADI 34 Saanya anatoa kadi za Njano kwa Banda na Yondani
MABADILIKO DK 30, Yanga wanamtoa DANNY MRWANDA na HUSSEIN JAVU anachukua nafasi yake
Dk 27 Singano anagongana na kipa Barthez, sasa anatibiwa...
Dk 24, Mrwanda na Kessy wanalambwa kadi za njano kutokana na faulo na kuchezeana kibabe.
Dk 21, Mwamuzi Said Juma Makapu analambwa kadi ya njano.
Dk 19, Tambwe anapiga kichwa mbele ya Murishid na mpira unapita juu ya lango la Simba
Dk 18, Msuva anaingia vizuri ndani ya eneo la 18 ya Yanga, lakini Murishid anaokoa.
Dk 14, Cannavaro anamuangusha Okwi aliyekuwa anakwenda langoni mwa Yanga lakini faulo aliyopiga Okwi inaishia miguuni mwa wachezaji wa Yanga.
Dk 9, Yondani anafanya kazi ya ziada kumzuia Okwi na kuondoa mpira huo.
Dk 8, Msuva anaingia kwa kasi, anamzidi mbio Mohammd Hussein na kupiga shuti dhaifu.
Dk 2, Ibrahim Ajib anakuwa wa kwanza kupiga shuti kali lakini linapita pembeni mwa lango la Yanga.
Dk 1 Mechi imeanza kwa kasi na Yanga wanakuwa wa kwanza kupata kona, lakini haina kitu
Comments
Post a Comment