Familia ya Mandela:'Ni kipindi kigumu'

Wananchi wa Afrika Kusini wamekuwa wakikesha kumkumbuka Mandela
Familia ya Hayati Nelson Mandela imezungumza kwa mara ya kwanza tangu Mandela Kufariki Alhamisi.
Wameelezea kuwa katika kipindi kigumu huku wakitarajia wiki moja inayokuja kuwa wakati mwingine mgumu kwao.
"Msingi wa familia yetu umetuondoka,’’ alisema msemaji wa familia ya Mandela Luteni Generani Themba Matanzima ingawa alisisitiza kuwa Mandela daima atasalia katika mioyo yao.

Watu wameendelea kukesha nchini Afrika Kusini huku wakimkumbuka Mandela.
Msafara wa magari utakaobeba mwili wake Mandela utapita katika barabara za Pretoria kwa siku tatu mfululizo kabla ya siku atakapozikwa Mandela Jumapili tarehe 15.
Maafisa watatangaza wakati msafara huo utakapoanza.
Mandela alifariki Alhamisi usiku akiwa na umri wa miaka 95 nyumbani kwake Kaskazini mwa Johannesburg
Mamia ya waombolezaji walikusanyika nje ya nyumba ya Mandela na kuwasha mishumaa usiku kucha wakiimba nyimbo za kusherehekea maisha ya Mandela.
Luteni Generali Matanzima alimfananisha Mandela na mti wa Mbuyu ambao uliwapa kivuli jamaa na familia yake.

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

NINI MAANA YA MAPENZI

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU