Wimbo wa STAMINA ft. CRISS WAMARYA “Mngekuwepo” umetolewa kimakosa bila ruhusa ya Stamina

STAMINA
Wimbo wa Stamina Ft Criss Wamarya unaoitwa Mngekuwepo umetoka kimakosa, jana wimbo huu uliwekwa hapa katika website hii mda huu nimetoka kupigiwa simu na Stamina na kuniambia huu wimbo
haujatoka kabisa wala hakuwa na plani ya kutoa wimbo huu, Stamina anasema wimbo huu ulikuwa unatakiwa uwe kwenye album na sio wakutolewa. Wimbo ambao alikuwa anatakiwa kuutoa ni mwingine kabisa na utatoka wiki ijayo, Stamini anawaomba radhi mashabiki wake kwa kitendo hiki cha kutolewa huu wimbo na mtu asiyemjua kabisa.
NOTE: Please wimbo huo usichezwe sehemu yoyote umetoka kimakosa

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

NINI MAANA YA MAPENZI

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU