Kocha wa Wales kujadili Mkataba wake leo
Kocha wa timu ya soka ya Wales
Chris Coleman atakutana na maafisa wa chama cha soka cha Wales hii leo
kujadili kuhusu mkataba mpya.
Coleman ambaye mkataba wake unamalizika baada ya
mchezo kati ya Wales na Finland tarehe 16 mwezi Novemba, ameelezwa
kupigiwa pande kuziba nafasi iliyo wazi kwenye timu ya Crystal PalaceMsemaji wa chama cha mpira cha Wales amesema kuwa wanaona kuwa zoezi la kuita mkutano wa waandishi wa habari hautakuwa na maana kwa kuwa maswali yatajielekeza kuhusu mkataba wa Chris na mipango ya kuhamia Crystal Palace.
Klabu ya crystal Palace ambayo Coleman amekuwa akiichezea kwa miaka minne imekuwa ikitafuta Kocha mpya baada ya kuondoka kwa Ian Holloway kuondoka mwezi uliopita.
Mkataba mpya wa Coleman utakuwa kwenye ajenda katika mkutano kati yake na maafisa wa Chama cha soka cha Wales zikiwa zimebaki siku nane pakee kabla ya mkataba wake wa sasa kumalizika.
Comments
Post a Comment