WAKAZI WA MBEYA WAJITOKEZA KWA WINGI KWENYE FURSA YA VIJANA NDANI YA TEKU.
Sehemu
ya vijana waliojitokeza kwa wingi kwenye semina hiyo ya Fursa kwa
vijana wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa ikijadiliwa ukumbini
humo.
Muwakilishi
wa NSSF-Makao Makuu Bwa,Salim Khalfan akizungumza mbele ya vijana
mbalimbali waliojitokeza kwenye semina ya Fursa kwa vijana,iliofanyika
mapema leo kwenye ukumbi wa chuo cha Teofilo Kisanji kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya. Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil,TPSF.
Mmoja
wa Vijana Wajasiliamali ,ambaye ana mradi mkubwa wa kuuza juisi,Gasto
Sony mkazi Uyole mkoani Mbeya,akieleza zaidi kwa vijana wenzake
waliojitokeza kwa wingi kwenye semina hiyo,namna ambayo ameweza kuitumia
fursa alioipata na kuwa mjasiliamali wa kuuza juisi kisasa kabisa.
Mkurugenzi
wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Eprahim Mafuru akizungumza
na wakazi wa Mbeya (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye semina ya
Fursa kwa vijana,filiofanyika leo asubuhi ndani ya ukumbi wa chuo cha
Teofilo Kisanji (TEKU),kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani
Mbeya.Kampuni ya Serengiti ndio wadhamini wakuu wa tamasha la Fiesta
2013 linalotarajiwa kufanyika jioni ya leo kwenye uwanja Sokoine.
Baadhi
ya vijana mbalimbali kutoka ndani ya mkoa wa Mbeya wakifuatilia mada
mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo mapema leo asubuhi
kwenye ukumbi wa chuo cha Teofilo Kisanji kilichopo maeneo ya Block
T-Mama John mkoani Mbeya.
Semina ya Fursa kwa vijana ikiendelea
Mkali
wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akifafanua jambo mbele ya
wakazi mbalimbali wa mji wa Mbeya,alipokuwa akiielezea mada mojawapo
iliyohusiana na fursa mbalimbali zilizomo ndani ya mkoa huo namna ya
kuzitumia,Semina hiyo imefanyika leo ndani ya ukumbi wa chuo cha Teofilo
Kisanji kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Eprahim Mafuru
akizungumza jambo na msanii wa muziki wa kizazi kipya aitway Niki wa
Pili ndani ya semina ya Fursa kwa vijana.
Muwakilishi
kutoka shirika la TPSF,Bwa.Louis Accaro akifunguka kuhusiana na mambo
ya fursa kwa vijana na nanmna ya kuzichangamkia mara zipatikanapo.
Mdau
wa Kilimo kutoka mkoani Mbeya,Bwa.Yona Daniel akizungumzia fursa
zinazopatikana kwenye kilimo,ambapo amewaasa vijana kujitokeza kwa wingi
kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye suala zima la
kilimo.
Semina
ya Fursa kwa vijana ikiendelea.Semina kama hii imekweíshafanyika kwenye
mikoa ya Kigoma,Singida,Tabora,Mtwara na leo mkoani Mbeya.
Comments
Post a Comment