WACHEZAJI WALIOMCHONGEA KUFUTWA DI CANIO
Inaarifiwa wachezaji wa
Sunderland walilalamika kwa mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Margaret Byrne
kuhusu kocha Paolo Di Canio kabla ya kupigwa kalamu.
Di Canio aliitisha mkutano wa timu nzima siku ya
Jumapili ambao inasemekana ulikumbwa na majibizano makali kufuatia timu
hiyo kushindwa mabao 3-0 na West Bromwich Albion...
.
Baadae wachezaji waandamizi
walimwambia Byrne kwamba hali imekua isioweza kuvumilika kwa sababu ya
tuhuma kali na matusi ya Mtaliana huyo dhidi ya kikosi cha timu hiyo.
Kikosi hicho ambacho hujulikana kama 'The Black
Cats' wameambua pointi moja tu kutoka mechi tano za ligi ya Premier
League katika msimu huu.
Aliyekua kocha wa Chelsea na West Brom Roberto
Di Matteo ndie anaetabiriwa na wengi kuteuliwa kuwa kocha mpya na
wengine wanaotajwa ni Gus Poyet, Tony Pulis na Alex McLeish.
Kocha msaidizi Kevin Ball ameteuliwa kua kaimu kocha kwa hivi sasa.
Di Canio ameshinda mechi 3 tu kati ya 13 baada ya kupigwa kalamu Martin O'Neill mnamo mwezi wa Machi.
Comments
Post a Comment