MCHUNGAJI WA KANISA LA EAGT JIJINI MBEYA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 NA VIBOKO 12 BAADA YA KUBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI
MCHUNGAJI WA KANISA LA EAGT JIJINI MBEYA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 NA VIBOKO 12 BAADA YA KUBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI
MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 baada ya kukutwa na makosa mawili ya Kubaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa miaka 19.
Akisoma
 hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Mbeya Ndugu Gilbert Ndeuruo
 amesema Mahakama imemtia hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na 
Shahidi namba moja katika kesi hiyo ambaye ni mhanga wa tukio hilo Neema
 Beni(19).
Amesema
 Mtuhumiwa huyo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mwezi Januari 2008 
hadi Mwaka 2011 katika eneo la Iwambi kinyume na Sheria kifungu cha 
130(2)e na 131 (1) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 
kwa kosa la ubakaji.
Kutokana
 na ushahidi huo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mahakama yake imemkuta 
Mtuhumiwa na makosa mawili ya Ubakaji na kumpa ujauzito kwa ushahidi 
uliotolewa na Mhanga mwenyewe pamoja na Mwalimu wa Shule aliyokuwa 
akisoma ambapo alidai kuwa Shitaka limedhihirishwa pasipo shaka chini ya 
kifungu cha 235/1985.
Kwa
 upande wake Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa aliiomba 
Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kutokana na mtuhumiwa kutenda kosa la 
kinyama tofauti na umri wake na wa binti ambapo Binti anaumri wa Miaka 
19 ili hali Mtuihumiwa akiwa na Miaka 57.
Pia
 alidai kuwa Mtuhumiwa huyo alimharibia masomo na maisha yake binti huyo
 na vitendo hivyo alikuwa akivifanyia sehemu mbali mbali ikiwemo 
kanisani , hivyo aliiomba mahakama hiyo kuvitaifisha na kutoa amri ya 
Matunzo ya Watoto kwa kutumia amri ya kutaifisha.
Hata
 hivyo Hakimu alimuuliza Mtuhumiwa kuhusu kupunguziwa adhabu ambapo Mshtakiwa 
huyo aliomba kupunguziwa adhabu kwa madi kuwa ameachiwa watoto na ndugu 
zake aliozaliwa nao wakiwemo wazazi wake hivyo akifungwa hawatakuwa na 
msaada.
Aidha
 kutokana na utetezi huo Hakimu Ndeuruo alimhukumu kifungo c ha Miaka 30
 na viboko 12 kutokana na kosa la kwanza ili hali katika kosa la pili 
amehukumiwa kifungo cha Miaka 5 na kuongeza kuwa adhabu hizo zitaenda 
kwa pamoja na kulipa fidia ya Shilingi Milion 20 kwa fedha za Tanzania 
kwa familia ya Mhanga.
Ameongeza
 kuwa Mtuhumiwa anahaki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu ya Mbeya 
kama hatakuwa ameridhika na adhabu aliyopewa na mahakama yake.
MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa mahakamani kungojea kesi yake.

Wananchi
 Mbalimbali wakisubiri Kusikiliza Kesi ya MCHUNGAJI wa Kanisa la 
Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya 
Daniel Mwasumbi
   MCHUNGAJI
 wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi 
Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi aliye vaa koti Jeupe   akiwa anatolewa 
mahakamani Baada ya kusomewa kifungo cha Miaka 30 Jela

  Watoto
 wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of 
Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa wanatoka 
Mahakamani Baada ya Baba yao kusomewa kifungo

  Mtoto
 wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of 
Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa anaongeaa na
 waandishi wa Habari baada ya kesi kumalizika

 Waumini Mbalimbali wakiwa nje Baada ya kesi kumalizika

Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa nje hawaamini baada ya kusikia Baba yao anafungwa Miaka 30
 Binti  anaye daiwa kufanyiwa kitendo hicho akilia kwa Uchungu baada ya kesi kwisha
  Binti  anaye daiwa kufanyiwa kitendo hicho akilia kwa Uchungu baada ya kesi kwisha

 
Comments
Post a Comment