MASHAIRI YA ONE DA INCREDIBLE YAKO HAPA


                                                                     VERSE 1
Hii ni news kwa ma – rap star/
Kwenye mdundo mi ni bao, nateleza na nina ujuzi wa kunata/
Utunzi bado culture, na – peruz kurasa/
Mwenyeji vituo vyote kama mluzi wa kondakta/
Uhh.. Beat ya Den texas/
Nchi ya verse, tenzi hazihesabiki hata kwa census/
Sense sick, spit ka` na – desease kwa senses/
New era muzik, Old rapper hit the benches/
Nawakilisha illmatix toka enzi/
Ikiwekwa beat kati tunagawa kama chenji/
Peace kwa J ryde, Bano Stylez enzi,
Toka tunafanya freestyle kwa ringtone za dre beats/
Tenzi za roho kutoka kwa rap dayosis/
Niko sick, sitibiki kwa anti-biotics/
Maabara ya mziki na – deal na rap science/
Uno the Chemist, Niko na text the Mad scientist…
VERSE 2
Check…. Hii ni for the people wa kitaa, People wa mitaani/
The people behind bars wanaoishi kwa imani/
Mother kani – teach tuko equal so sidhani…./
…. Ka` nikiku – treat sivyo tutakuwa people wa amani/
Sikupeleki higher nakurusha/
Haina ku – retyre, weka fire kama kaya kwa wavuta/
Namwaga dawa ka` supplier, ama pusher/
Mpaka wanachoka mbaya, shonea waya kwenye bukta/
Mbaya nawakilisha/
Hata nibarikiwe na uhai wa kujidai mpaka Messiah anapofika/
Na sina ubaya, nimeutumia mpaka umekwisha/
So, hata niki – retyre nitaimba kwaya ya kanisa/
We ni Big screen star unaetisha/
Mi ni sixteen bars za sifa, hapa u – star unakwisha/
Muda hausimami, masaa yanapita/
Maisha ni movie ya kila siku, mi ni star kwenye picha…
VERSE 3
Hii sio Hip Hop conscious, ni hoja njema/
Sina nguzo tano, mi natumia moja vyema/
Moja tena, niite nyota njema/
Ka` ulie nae mikosi huna budi kumngoja Mwema/
Bado mbinde nilinde hali/
Mkali jilinde, kama unaringa kibingwa karinge mbali/
Jilinde na zali, habari zifike kwa wahuni wa maskani, niko nanyi kama vizinde vya kali/
Sina drama wa beef kumbuka/
Hizo peleka kwa baby – momma, sio sisi utaumbuka/
Huu ndo mwanga, mweusi hawezi wanga, hapa zina twangwa chungu sio rahisi kumumusa/
Ukihisi nimekugusa, Diss/
Hizi flo kubwa zinawavuka, iwe bukta ama jeans/
Stuka ama sizi/
Sanuka hawa machizi wameshafua, na hawawezi kukauka zama hizi

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU

NINI MAANA YA MAPENZI