YANGA HII MTAIKOMA


 Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji.
Wilbert Molandi,
Dar es SalaamYANGA ina mipango we acha tu, kwani inasubiri Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litoe kauli yake ya kuruhusu matumizi ya wachezaji kumi wa kigeni katika vikosi cha Ligi Kuu Bara halafu ifanye kufuru.
Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm, raia wa Uholanzi, aliliambia Championi Jumamosi kuwa, akiruhusiwa tu kutumia nyota kumi basi wapinzani wake kazi wanayo.
“Na wataikoma Yanga itakayopatikana kupitia usajili utakaofanyika,” alisema Pluijm huku akiwa ameshika tumbo lake na kutabasamu. Yanga tayari ina wachezaji watano wa kigeni ambao ni Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima (Rwanda), Andrey Coutinho (Brazil), Kpah Sherman (Liberia) na Amissi Tambwe wa Burundi.
Katika kuhakikisha inashiriki ipasavyo msimu ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika na ligi kuu, tayari Yanga imesajili wachezaji wa ndani, winga Deus Kaseke kutoka Mbeya City, beki wa kati Haji Mwinyi (KMKM), kipa Benedict Tinoko (Kagera Sugar) na Malimi Busungu kutoka Mgambo JKT.
Kamara.
Bosi mmoja mwenye fedha na nguvu ya usajili ndani ya Yanga, amelisisitizia gazeti hili: “Hapa tunasubiri TFF iseme tu kama tunaruhusiwa kuongeza hao wageni ili tuwasajili wote tunaowataka na mtaona kikosi chetu.”
Alisema mchezaji wa kwanza kusajiliwa atakuwa straika Donald Ngoma wa FC Platinum ya Zimbabwe, halafu atafuata kiungo Lansana Kamara wa Sierra Leone ambaye anafanya majaribio na wachezaji wawili kutoka Ghana ambao wanaletwa na Pluijm. “Kama huyo Ngoma kila kitu kipo sawa ila tunasubiri uhakika wa wachezaji kumi wa kigeni,” alisema bosi huyo kwa kujiamini.
Championi Jumamosi linafahamu kwamba TFF itapitisha maombi hayo ya matumizi ya wachezaji kumi wa kigeni kutumika kwani klabu zenye nguvu za Simba, Yanga na Azam, sasa zipo mstari wa mbele kupitisha kanuni hiyo.
Hata hivyo, endapo mpango huo utakwama, Yanga inapanga kutazama upya mchezaji wa kumpunguza katika orodha ya wageni ambapo panga zaidi litawaelekea Coutinho na Sherman.
Simon Msuva.
“Ndiyo maana tupo kimya hapa tunasikilizia kwanza kwani tunaogopa kuingia hasara ya kumsainisha mchezaji halafu tukakwama jinsi ya kumtumia,” alisema bosi ambaye ni ‘stelingi’ wa usajili wa kimafia Yanga. Kwa mujibu wa Pluijm, leo Jumamosi Yanga itafanya mazoezi ya kujenga stamina kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la jirani na Hospitali ya Aga Khan.
Kamati ya Mashindano ya TFF inayoongozwa na Geofrey Nyange ‘Kaburu’ na makamu wake Clement Sanga, itakutana Juni 20, mwaka huu kupitisha au kukataa ombi hilo. Kaburu ni makamu wa rais wa Simba na Sanga pia ana cheo hicho kwa Yanga.
Mambo yakienda sawa Yanga itakuwa na nyota kibao ambao ni Kaseke, Simon Msuva, Tambwe, Ngoma, Kamara, Busungu na wengineo.
JIUNGE NA MICHEZO KIGANJANI TUMA NENO SPORTS KWENDA NAMBA 15778






Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU

UMUHIMU WA KUJIFUNZA SAIKOLOJIA