KITUNGUU SWAUMU KINGA YA MAGONJWA MBALIMBALI

Tafiti nyingi zimeshafanyika duniani kuhusu faida za kitunguu swaumu ambazo zimethibitisha kuwa mtu akitafuna na kumeza hata punje moja tu ya kitunguu swaumu kila siku asubuhi, basi mtu huyo atakuwa amejitengenezea kinga ya mwili ya kudumu itakayomlinda na maradhi mbalimbali, yakiwemo maradhi sugu yaliyoshindikana hospitalini.
Kitunguu swaumu kimegundulika kuwa rafiki wa damu mwilini, kwani kinapoliwa, huenda moja kwa moja kutoa sumu zote kwenye damu na kuipa damu vitamin na huongeza uwezo wa damu kusafiri vyema katika mishipa hivyo kumfanya mtu ajisikie mwenye afya njema kila siku.
Aidha, kitunguu swaumu kimegundulika kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia magonjwa ya moyo
kwa kupenya katika mishipa ya damu na kuvunja-vunja Cholestrerol zote ili kupisha njia ya damu iwe safi na wazi kutokana na ‘antibiotic’ iitwayo ‘Allicin’ iliyomo kwa wingi katika chakula hiki.
China na India zinaaminika kuwa ni nchi ambazo wakazi wake ni watumiaji wakubwa wa kitunguu swaumu katika milo yao ya kila siku. Tabia hii imewasaidia sana kujikinga na maradhi mengi yanayoweza kuzuilika. Bila shaka hata Watanzania tukiamua kutumia kwa wingi kitunguu hiki katika milo yetu ya kila siku, tutajikinga na maradhi mengi na hata  uwezo wa kufikiri (Extra clear thinking capacity) utaongezeka, kwani kitunguu huongeza akili pia.
Ili nawe kujiepusha na maradhi na pengine kuyatibu yale ambayo umeshayapata kwa kutumia njia asilia, tafadhali anza sasa utaratibu wa kutafuna na kumeza angalau punje moja tu ya kitunguu swaumu kila siku asubuhi kabla ya kula chochote, fanya kuwa utaratibu wako wa kila siku. Ili kuondoa harufu mdomoni, tafuna kwanza kisha kapige mswaki na kuendelea na mlo wako wa kawaida.
Kuna jambo ambalo linaweza kuwakatisha tamaa ya kupona baadhi ya watu watakaotumia kitunguu swaumu kama dawa. Tafiti zimeonyesha kuwa upo uwezekano wa baadhi ya vitunguu swaumu kutokuwa na virutubisho vinavyotakiwa. Hii inatokea, na inahusisha sana aina ya udongo uliyopo mahali kilipooteshwa kitunguu hicho na kwa akili ya kawaida, utakubali kuwa kile kilichoota kwenye udongo wa mfinyanzi hakitakuwa na ladha sawa ya kile kilichoota kwenye mchanga.
Kwa kutambua hilo, watafiti waliamua kutengeneza vidonge vya vitunguu swaumu ambavyo tayari vimepitishwa katika maabara kuhakiki ubora kabla ya kusindikwa na kutengezwa vidonge vyenye uhakika wa tiba. Vidonge hivyo vipo madukani na ukivihitaji utapewa maelekezo ya kuvipata kwa kuwasiliana na mwandishi wa makala haya.

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU

UMUHIMU WA KUJIFUNZA SAIKOLOJIA