Siku tatu za maombolezo zaanza nchini Kenya baada ya oparesheni dhidi ya magaidi katika jengo la Westgate kutamatika


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, akiwahutubia wananchi wa Taifa hilo
REUTERS/Presidential Strategic Communications Unit


Wananchi wa Kenya hii leo wameanza maombolezo ya siku tatu kama ilivyotangazwa na Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, maombolezo hayo yanakuja baada ya kutamatika kwa opersehni nzito ya kuwakabili magaidi walioteka jengo la maduka la Westgate toka siku ya jumamosi mwishoni mwa juma lililopita.

Kwenye hotuba yake iliyodumu kwa karibu dakika sitini Rais Kenyatta amevipongeza vikosi vya Kenya vilivyoshiriki kwenye operseheni hiyo pamoja na ushauri wa mataifa ya Afrika na Magharibi ambao walishiriki kuhakikisha uasi kwenye jengo la Westgate unatamatishwa.
Aidha Kenyatta amewashukuru wananchi wa Kenya kwa ushirikiano waliouonesha toka mwanzo hadi mwisho wa operesheni yenyewe akieleza kufurahishwa na namna watu walivyojitokeza kuchangia damu bila kujali eneo wanalotoka wala utaifa wa wahanga wa tukio la westgate.
Kenyatta amewahakikishia raia wake ulinzi wa kutosha na kuongeza kuwa taifa hilo ni salama na wananchi wala wageni wasiwe na hofu.
Katika hatua nyingine, naibu waziri mkuu wa Somalia ambaye pia ni waziri wa mambo ya kigeni wa taifa hilo, Fawzia Yousouf Haji Adam, amesema nchi yake inawashukuru wananchi wa Kenya pamoja na wanajeshi wa taifa hilo kwa kufanikisha kurejesha usalama nchini mwake na kwamba tukio hili linaonesha namna ambavyo Kenya iko tayari kukabiliana na ugaidi.
Lakini wakati operesheni hii ikikamilika bado kuna maswali mengi yanayohitaji majibu kuhusu namna operseheni hiyo ilivyoendeshwa na matukio ya mwisho kwenye operseheni hii huku kukiwa na hofu kuwa idadi ya watu waliouawa kwenye opersheni hiyo huenda ikaongezeka zaidi.
Wakati huo huo Rais wa Ufaransa, Francois Hollande ametoa wito kwa viongozi wa dunia kuhakikisha nchi zao zinapambana na makundi ya kigaidi ambayo yameendelea kuwa kitisho cha usalama wa dunia.
Akiwa mjini New York Marekani katika mkutano wa 68 wa Umoja wa Mataifa Rais Hollande amegusia tukio la nchini Kenya na kuongeza kuwa ni ishara tosha kuwa makundi ya kigaidi yanaendelea kupata nguvu na kuua wau wasio na hatia.
Rais Holande pia amegusia uasi unaoshuhudiwa kaskazini mwa nchi ya Mali na kudai kuwa nchi yake itahakikisha inatoa ushirikiano wa kutosha kwa nchi ya mali na nchi washirika kukabiliana na makundi ya kigaidi.

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU

UMUHIMU WA KUJIFUNZA SAIKOLOJIA